Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Mapigano yasitisha safari za ndege mjini Sanaa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Ripoti kutoka mji mkuu wa Yemen Sanaa zinasema safari za ndege zimesitishwa kwa muda katika uwanja wa ndege wa Sanaa huku mapigano yakipamba moto karibu na uwanja huo. Kiasi ya watu 15 wameuwawa kwenye mapigano yaliyoendelea usiku kucha jana kati ya wapiganaji wa kikabila wanaomuunga mkono Sheikh Sadeq al Ahmar ambao walimiminika kuelekea mji mkuu, na wanajeshi wa rais Ali Abdullah Saleh. Afisa mmoja wa safari za ndege aliyenukuliwa na AFP amesema ndege zinaelekezwa uwanja wa Aden, ambao ni mji wa kusini mwa Yemen.


Walioshuhudia wamesema maelfu ya watu wamekimbia kutoka Sanaa, maduka yamefungwa, na kuna milolongo mirefu katika vituo vya mafuta ya petroli. Mapigano yalizuka siku ya jumanne baada ya kuporomoka kwa makubaliano ya kuweka chini silaha ambayo yalipatanishwa na mataifa ya Ghuba. Katika mji mwingine wa kusini Taez, walioshuhudiwa wamesema wanajeshi wa Yemen kwa mara nyengine wamewafyatulia risasi waandamanaji , ambao wamekuwa wakimtaka Saleh ajiuzulu.

0 comments

Post a Comment