HAKIMU Mkazi wa Mahakakama ya Hakimu Mkazi Arusha , Charles Magesa ameomba apewe muda wa kutosha ili ajiridhishe na maelezo ya upande wa mashtaka kwamba afute dhamana kwa viongozi wa Chadema na wafuasi wao baada ya kushindwa kutokea mahakamani Mei 27, mwaka huu.
Hakimu Magesa alisema maelezo ya upande wa mashtaka na utetezi yalikuwa marefu na kwamba anahitaji muda mrefu zaidi wa kupitia maelezo hayo na kwamba sasa atatoa uamuzi sahihi Juni 2, mwaka huu.
Wakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo ni Method Kimomogoro na wakili upande wa mashtaka ni Edwin Kakolaki wakati washtakiwa ambao hakuudhuria mahakamani ni Phillimon Ndesamburo, Godbless Lema, Freeman Mbowe na Joseph Selasini.“Naahirisha kesi hii mpaka Alhamisi wiki hii asubuhi saa 5:00 na hapo nitatoa uamuzi wangu, kuhusu mvutano huu wa dhamana,” alisema Magesa.
Akijibu hoja za upande wa utetezi wakili Kakolaki aliiambia mahakama kuwa hajaridhishwa na sababu zilizotolewa baada ya washtakiwa kutokuwapo mahakamani Mei 27, mwaka huu.
Kakolaki alisema hakubaliani na hoja ya wakili wa utetezi Kimomogoro kwamba mahakama ilitoa idhini Aprili 29, mwaka huu ili washtakiwa wasiudhurie mahakamani Mei 27, mwaka huu kwa sababu
wabunge watakuwa wakiudhuria vikao vya kamati za bunge.
Alifafanua kwamba hoja ya wabunge kuudhuria vikao vya bunge haina msingi na kamwe hakubaliani nayo.“Sikubaliani na hoja hizo kwa sababu mahakama ilitoa amri hawatakuwepo ila lazima wawepo wadhamini wao, sasa hii ni dharau kwani hawakuleta hata wadhamini wao, hivyo naomba waondolewe dhamana kwani hoja zilizotolewa hazina msingi wowote,” alisema wakili Kakolaki.
Kuhusu mshtakiwa Freeman Mbowe na Phillimon Ndesamburo, alisema hawastahili kuwekewa dhamana kwa sababu waliidharau mahakama kwa kutofika mahakamani Mei 27, na Mei 30, mwaka huu.
Wakili Kakolaki alisema kuhusu Mbunge Godbles Lema kwamba alishindwa kufika mahakamani kwa kuwa alikuwa kwenye kamati ya bunge siyo ya kweli kwa sababu hakuwepo katika kamati yoyote na alidharau mahakama.
“Ila kwa sababu alikuja mahakamani jana Mei 30, sina mashaka naye na hata Dk Wilbroad Slaa, naye sina tatizo naye, isipokuwa sababu ya Dk Slaa ya kuaribikiwa gari njiani huko Same siku ya kesi, siyo kweli kwa sababu siku hiyo jioni Mei 27, mwaka huu alionekana katika luninga ya TBC akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) jijini Dar es Salaam,” alisema Kakolaki.
“Kwa mshtakiwa Richard Mtui sina tatizo naye kwa sababu alituma mdhamini wake kuja mahakamani, japo naye hajaonyesha cheti cha kama alikuwa anaumwa ugonjwa wa kisukari, hivyo kuna mashaka hapo,” alisema Kakolaki.
Kakolaki aliendelea kupinga sababu za wakili Kimomogoro kwamba Aprili 29, mwaka huu walipeleka cheti cha hospitali ya Muhimbili kuonyesha kwamba ni mjamzito wa miezi minane na atajifungua muda mfupi ujao ila cha kushangaza Jana Mei 30, walileta cheti kinachoonyesha tena ana mimba ya wiki 30 huku akidai kuwa ina maana ya kuwa mimba hiyo ni ya miezi saba na kusisitiza huo ni uongo.
“Huu jamani ni uongo wa hali ya juu, kwa sababu mimba inaenda mbele siku zote hairudi nyuma, kutokana na sababu hii napinga na pia hata mdhamini wake alitakiwa kuja kutoa sababu mahakamani hajafika,” alisema Kakolaki.
Alisema kutokana na sababu zilizotolewa hakubaliani nazo na anaomba mahakama itoe onyo kwa washtakiwa hao ila kwa Ndesamburo na Mbowe wakamatwe kwa kudharau mahakama.
Kwa upande wake wakili Method Kimomogoro, baada ya kupewa nafasi ya mwisho na Hakimu, aliiomba mahakama, kutupilia mbali maombi ya wakili huyo wa serikali kwa sababu hayana msingi.
"Mimi naendelea kusema kutokana na sababa ya idhini iliyotolewa mahakama Aprili 29, mwaka huu, ndiyo sababu ya msingi ya washtakiwa kutofika mahakamani na pia mbunge Lema sababu iliyokataa hakuwapo kwenye kamati siyo kweli na kama wakili angehitaji ajue alikuwa katika kamati gani angeomba na akapewa maelezo na siku hiyo walikuwa mawakili watatu wa serikali kwa nini hawakuhitaji waelezwe kwamba mbunge alikuwa katika kamati gani,”alihoji Kimomogoro.
Aliomba mahakama hiyo kuendelea na kuwaachia huru kwa dhamana zao za awali washitakiwa kwa sababu ni watiifu na kuhusu suala la cheti cha Richad Mtui kuwa hana ugonjwa wa kisukari, siyo kweli kwani wakili huyo kama angekihitaji chati hicho angekifuatilia katika hospitali husika na angekipata cheti hicho.
“Josephine Slaa, mimi nasema hii inachekesha kuona wakili wa serikali haamini cheti cha hospitali ya Muhimbili chenye miezi miwili tofauti ya mimba, wakati hiyo hiyo hospitali ndiyo iliyompasua mtu kichwa badala ya mguu haya ni matokeo ya serikali kutotoa vifaa vya kisasa vya wafanyakazi wa hospitalini, hivyo hiyo sababu haimuhusu mteja bali ni suala la hospitali” alisema Kimomogoro na kuibua kicheko kwa watu waliohudhuria mahakamani hapo.
Aliendelea kuiomba mahakama iwaruhusu washtakiwa kuwa nje kwa dhamana kwa sababu ni watiifu.Kesi hiyo imehairishwa na Hakimu Magesa mpaka Juni 2, mwaka huu itakapotolewa uamuzi wa dhamana za washitakiwa hao.
Awali washtakiwa ambao ni viongozi wa Chadema Taifa na wafuasi wao 19, walishtakiwa kwa kosa la kukusanyika bila kibali na kutoa matamshi ya uchochezi na kuhatarisha amani.

0 comments