Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Sakata la Mara, Nahodha atupa lawama kwa Barrick

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, amesema mauaji ya raia yaliyotokea mgodi wa North Mara, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, yamesababishwa na ahadi za uongo zinazotolewa na wawekezaji kwa wananchi. Akizungumza kwenye kipindi cha maswali na majibu cha dakika 45, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV juzi, Nahodha alisema tayari  amefanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ili kulifanyia kazi suala hilo.

Nahodha alisema makubaliano yake na Ngeleja, ni kutafuta muda wa kwenda kwenye mgodi huo ndani ya wiki mbili zijazo, kwa lengo la kuhakikisha kunakuwapo hali ya utulivu, ikiwamo wawekezaji kutekeleza ahadi walizotoa kwa wananchi hao.

”Kitendo hicho kinawezekana kimetokea kutokana na huduma za jamii kuwa ndogo kwenye eneo lile, kwa hiyo wawekezaji wanatoa ahadi kuwasaidia wananchi, lakini hazitekelezwi,” alisema Nahodha na kuongeza: ”Vijana waishio maeneo yale wanaona wawekezaji wananufaika wenyewe na wao kubakia maskini.” Kuhusu vitendo vya mauaji nchini yanayofanywa na polisi, Nahodha alisema Tanzania upo utamaduni wa kila mmoja anataka kujichukulia sheria mkononi, hali ambayo siyo nzuri.

Alishauri iwapo raia anahisi hajatendewa haki, kufuata ngazi nyingine kama Tume ya Haki za Binadamu, wabunge na mahakama ambavyo viko kwa ajili ya kuisaidia jamii.

“Kwa kweli kila mtu akijichukulia sheria mkononi hakutakuwa na amani katika nchi. Katika sheria ya nchi sura ya 322, pPolisi amepewa mamlaka ya kumlinda raia na mali yake, lakini akikusimamisha ukaweka mkono mfukoni anachukua roho yako,” alisema. Kuhusu wimbi la kukamatwa kwa wabunge nchini, Nahodha alisema kinga za wabunge ziko wakati anapotekeleza wajibu wake na kwamba, hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria.  

0 comments

Post a Comment