IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kimepata njia mpya ya kuwadhibiti wafanyabiashara wanaojiunga na chama hicho na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa nia ya kuendeleza vitendo vya rushwa.
Hayo yalibainishwa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza katika mkutano wake wa hadhara uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua ya kujivua gamba.
Nnauye alisema ilifika maali wananchi walipoteza imani kwa chama na viongozi wake, jambo lililokisukuma chama kuchukua hatua za kurekebisha mambo.Alisema mambo hayo ni pamoja na kukomesha vitendo vya rushwa kwa wagombea na wanachama ili kukirudisha chama katika mstari unaotakiwa.
Katibu huyo wa uenezi, pia aliwataka madiwani wa CCM kote nchini kutowavumila na ikibidi kuwachukulia hatua za kinidhamu, baadhi ya watendaji wa serikali wanaokwamisha miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zao .
Alisema hayo jana kwa nyakati katika mikutano iliyofanyika katika Kijiji cha Majimoto na Usevya, wilayani Mpanda, akiwa katika ziara yake ya mkoani Rukwa na Katavi.
Alisema wananchi wanaichukia CCM kwa sababu baadhi ya watendaji wa serikali hawataki kutekeleza ilani ya CCM.Alisema kwa kuzingatia hali hiyo uongozi wa CCM umeamua kupambana na watwendaji hao katika halmashauri zote na kwamba madiwani wa CCM, wajibu wao kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watu hao.
"Kuna baadhi ya watendaji wa serikali katika ngazi za mikoa wanakwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoko katika ilani ya CCM sasa kamwe hatuwezi kuwavumilia na wale wanaojifanya miungu watu kwa kuwanyanyasa wananchi kiasi cha kuichukia CCM hawapaswi kuvumiliwa," alisema Nape.
Akizungumzia safari za nje alizofanya Rais Jakaya Kikwete, na ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wapinzani alisema zimesaidia nchi kupata misaada mikubwa
You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - 'CCM imepata njia ya kuwadhibiti mafisadi'
0 comments