UCHAGUZI wa viongozi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana ulitawaliwa na vituko vilivyoambatana na wagombea wa nafasi ya mwenyekiti, kuwekwa chini ya ulinzi mkali, ili kuwadhibiti wasitoe rushwa kwa wapiga kura. Vituko hivyo vilitokea katiKa mkutano huo wa uchaguzi ulioanza saa 6:00 mchana, katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam na kuendelea hadi usiku.
Katika uchaguzi huo, wagombea tisa wa nafasi ya mwenyekiti, walitolewa nje ya ukumbi wa mkutano na kuwekwa chini ya ulinzi wa mkali wa mabaunsa wawili.Kitendo hicho kilifanyika wakati wagombea hao, wakisubiri kuitwa kwa mahojiano yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wa chama.
Chini ya ulinzi huo, wagombea hawakuruhusiwa kwenda mahali na hata pale walipoitwa kwa mahojiano, walisindikizwa hadi mlangoni.

Mapema uongozi wa Chadema ulipiga marufuku, wagombea wote kufanya kampeni nje ya ukumbi wa uchaguzi.
Uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Bavicha unafanyika baada ya kushindikana kwa uchaguzi wa awali wa Septemba mwaka juzi, kufuatia vurugu kubwa zilizosababisha uongozi kuusimamisha.

Vurugu hizo zilimlazimisha aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi,Charles Mwera kushindwa kutangaza matokeo na hatua hiyo ilikuja baada ya kubainika kuwa upigaji kura, ulikuwa batili.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya kura zilizohesabiwa kuoenekana kuwa zilizidi idadi ya waliopiga kura hizo na hakukuwa na mgombea mmoja aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura.
Uchaguzi huo uliwapambanisha wagombea wengi, lakini waliokuwa wapinzani wa karibu ni aliyekuwa Ofisa Habari wa Chadema, David Kafulila na aliyekuwa Diwani wa Tarime Mjini, John Heche.Wagombea wengine walikuwa ni Ofisa wa Mafunzo, Day Igogo na Julieti Rushuli.
Uchaguzi huo wa jana uliwashirikisha wagombea wa nafasi za wajumbe wa Baraza Kuu la Vijana na Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chadema.Hata hivyo, akizungumza kabla ya uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilibrod Slaa, alisema baadhi ya majina ya wagombea yamekatwa kwa sababu ya kutoa rushwa kwa wapiga kura.
Dk Slaa alisema kuna ushahidi kwamba mmoja wa mgombea aliyeondolewa, alitoa rushwa kwa wapiga kura kutoka mikoani kwa kuwatumia fedha kwa njia ya M-pesa. Alisema chama hicho kimejipanga kuepuka vitendo vya ukiukaji wa maadili ikiwa ni pamoja na kutoa na kupokea rushwa.
"Tulikubaliana ndani ya kamati kuwa kampeni zote zitapigwa ndani ya ukumbi wa mkutano,"alisema Slaa. Alisema ni vyema kila mgombea afuate taratibu zilizokuwa na chama, ili kufanya uchaguzi uwe utulivu na wa heshima, hatua ambayo alisema itakijengea chama sifa.
Mkakati wa kuwadhibiti wagombea uliendelea hadi Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alipotangaza taratibu za kuanza kwa kampeni, ambapo wagombea wote waliamriwa kutoka nje ya ukumbi na kuruhusu mgombea mmoja mmoja kwa ajili ya kujieleza.
Waliokuwa wakigombea nafasi ya mwenyekiti ni na Aidan Sadick, Benard Mao, Benard Saanane, Deogratias Kisandu, Edwin Soko, Grayson Nyakarundu, John Heche, Masood Suleimani na Mtela Mwampamba.
Nafasi zingine zinazogombewa ni ya Makamu mwenyekiti bara, Makamu mwenyekiti visiwani, katibu mkuu, naibu katibu mkuu, na uratibu na uhamasishaji.Hatua hiyo ya Chadema kudhibiti rushwa inakuja wakati mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, akiwataka viongozi wasiwapitishe wagombea mamluki, kushika nyadhifa ndani ya chama hicho.
Mtei ambaye alitoa wito huo juzi, alisema Kamati kuu ya chama hicho, ilitakiwa kuwa ya kwanza kuchuja majina ya wagombea. Hadi tunakwenda mtamboni uchaguzi huo ulikuwa ukiendelea.
Kutohudhuria mahakamni
Akizungumzia sababu za kutokuhudhuria mahakamani juzi, Dk Slaa alisema ni makubaliano yaliyofikiwa baina yao na mahakama kuhusu kutokwenda mara kwa mara hadi hapo afya ya mmoja wa washitakiwa, itakapotengamaa.
"Nasikitika kuwa limetokea hili, lakini wote wanajua sisi ni viongozi wa watu wasioweza kutoroka. Jumatatu (kesho) mimi nitakwenda Arusha kuwasikiliza,"alisema Slaa.
Dk Slaa alisema tukio la juzi lilitokea baada ya kesi hiyo kutajwa saa 2:00 asubuhi badala ya saa 3:00 asubuhi.
Alisema kutokana na sababu hiyo wakili alikwenda mahakamani na kushughulikia kesi nyingine na alipokwenda kwenye kesi yao saa 3:00 asubuhi alikuta ikiwa imeshaahirishwa.
Kuhusu wabunge, alisema kwa sasa wametawanyika na wana majukumu ya kitaifa na kwamba hawatakwenda mahakamani Arusha."Mahakama imetoa amri ya mimi na wabunge kukamatwa, hata hivyo ni vigumu kuwapata wabunge wangu, mwenyekiti wangu atakuwa bungeni kupokea taarifa ya waziri mkuu,"alisema Dk Slaa .

0 comments