Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Ali Abdullah Saleh wa Yemen kuondoka ndani ya siku 30

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Waakilishi wa upinzani nchini Yemen, wametia saini makubaliano yaliyopendekezwa na nchi za Ghuba, yakimtaka Rais Ali Abdallah Saleh kuondoka madarakani katika kipindi cha siku 30 na badala yake hatofikishwa mahakamani.
Wizara ya Mambo ya Ndani imesema, wajumbe watano wa upinzani wametia saini makubaliano hayo mbele ya mabalozi wa kigeni. Kwa mujibu wa upinzani, miongoni mwa wageni hao ni wajumbe wa Marekani, Umoja wa Ulaya na Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi la Nchi za Ghuba.


Hii leo, Rais Saleh anatazamiwa kuidhinisha makubaliano hayo. Serikali ya umoja wa kitaifa itakayoongozwa na upinzani, inapaswa kuundwa katika kipindi cha wiki moja. Yemen imekumbwa na machafuko na maandamano dhidi ya Saleh, anaetawala kwa takriban miaka 33 nchini humo.

0 comments

Post a Comment