SIKU moja baada ya baadhi ya wanachama wa UVCCM Mkoa wa Arusha kufanya vurugu wakishinikiza Katibu wa CCM wa mkoa huo, Mary Chatanda ajiuzulu, kiongozi huyo amewajibu kuwa: "Sing'oki ng'o."Juzi, hali haikuwa shwari katika chama hicho tawala mkaoni Arusha baada ya gari la katibu huyo kunusurika kuchomwa moto na baadhi ya wanachama wa UVCCM.
Wanachama wa umoja huo kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha, waliandamana katika Jengo la Makao Makuu ya CCM mkoa huo wakishinikiza Chatanda na Mjumbe wa Baraza la Vijana la Mkoa, Mrisho Gambo 'wajivue gamba'.Hali hiyo ilitokea wakati Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa kikiendelea hali iliyosababisha dereva wa gari la katibu huyo wa CCM kulitoa nje ya jengo hilo.
“Sifikirii kujiuzulu na wala halinipi shida hilo, labda niamue kuandika barua ya kuomba uhamisho. Mimi sikuchaguliwa, niliteuliwa na taasisi za UVCCM, UWT, Jumuiya ya Wazazi zote ziko chini yangu hivyo sitishiwi nyau.”Chatanda alidai kuwa maandamano hayo yaliratibiwa na baadhi ya viongozi ambao hata hivyo, hakuwataja.
Alisema baadhi ya vijana wa UVCCM walishiriki maandamano hayo baada ya kupotoshwa na viongozi wao huku akidai kuwa anawatambua watu wote walioratibu maandamano hayo.
“Vijana walipotoshwa na viongozi wa umoja huo, nawatambua wote walioratibu maandamano hayo sitawataja kwa sasa lakini wote tutawashughulikia kupitia vikao vya kamati ya utendaji ya chama,” alisema Chatanda.Kuhusu madai kuwa alichangia CCM kupoteza Jimbo la Arusha Mjini, katibu huyo alisema: "Mimi nilikuwa mtendaji wa wilaya zote mkoani Arusha hivyo kama ni lawama, walipaswa kupewa aliyekuwa katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Salum Mpamba na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
"Kuhusu madai ya ofisi yake kuingilia uamuzi wa vikao vya umoja huo wa vijana, alisema kuwa kikao cha uamuzi cha umoja huo kilichofanyika wilayani Longido hivi karibuni, kilikiuka taratibu za chama na hakikuwa halali kwa mujibu wa taratibu za chama.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Milya alikanusha madai ya Chatanda kuwa baadhi ya viongozi wa umoja huo waliratibu maandamano hayo.Alisema maandamano hayo yalitokana na hisia za wanachama wa umoja.Milya alisema UVCCM hauwezi kumvumilia mtu ambaye amekuwa akikivuruga chama chao huku akiutaka uongozi wa CCM ngazi ya taifa usikilize kilio cha umoja huo kwa kumwondoa Chatanda.
“Tunakanusha kabisa. Maandamano hayo hayakuratibiwa wala kufadhiliwa na mtu yeyote, vijana wamebeba hisia za viongozi wao za kumtaka Chatanda aondoke.”Alimtupia lawama Chatanda akisema ndiye aliyesababisha Jimbo la Arusha Mjini liangukie upinzani akisema wakati wa mchakato wa kura za maoni, alikuwa Tanga akisaka nafasi ya ubunge wa viti maalumu kupitia mkoa huo.
"Hata baada ya kura za maoni alikuwa (Chatanda) na mgombea wake (hakumtaja) alikuwa akimpinga Dk Batilda Buriani aliyepitishwa na chama," alidai kiongozi huyo wa UVCCM.
Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema asingeweza kufanya hivyo kwa kuwa bado liko kwenye ngazi ya mkoa."Kila ngazi katika chama kuna vikao vyake. Kwa sasa bado liko (suala hilo) kwenye ngazi ya mkoa, nikiletewa tutakuwa na nafasi nzuri ya kulizungumzia ila kama hatujaletewa siwezi kusema chochote," alisema Nnauye.
Hata hivyo, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Sanare alipoulizwa maazimio ya kikao cha kamati ya siasa mkoa kilichokaa juzi kujadili suala la Chatanda na Gambo alisema kikao kiliazimia kulifikisha suala la Chatanda katika ngazi ya taifa huku la Gambo likirudishwa katika uongozi wa UVCCM kwa lengo la kumpa nafasi kada huyo ajieleze juu ya tuhuma zinazomkabili.

0 comments