BAADA ya sakata la yule Askofu Mkuu wa Kanisa la Apostle Majani la Namanga, Tegeta, jijni Dar es Salaam, Jamal Ally Hussein (pichani), kukumbwa na skendo ya kunaswa kitandani akiwa katika pozi na denti aitwaye Basilisa, ishu nyingine imemuibukia ambapo safari hii, picha zake zikimuonesha akiponda raha kwa kupiga mbizi ufukweni mwa Bahari ya Hindi zimedakwa na Risasi Jumamosi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kilizidaka picha hizo, mtumishi huyo alikwenda ‘kujirusha beach’ kufuatia kazi ngumu ya kuwachunga kondoo wa Bwana ambao wengine ‘hawachungiki’ kutokana na ugumu wa mioyo yao.
Katika picha hizo, Askofu Jamal akiwa kifua wazi anaonekana na wanawake wengine wawili, kulia na kushoto kwake.
Kama hiyo haitoshi, kiongozi huyo wa kiroho anaonekana akiogelea kwa staili mbalimbali, hali iliyoashiria umahiri wake katika kukaa majini kwa muda mrefu.
Katika picha hizo, mbali na Askofu Jamal, jirani yake anaonekana mwanaume mwingine, naye akiwa na wanawake wawili kulia na kushoto kwake.
Haikujulikana mara kama mtumishi huyo wa Mungu ana uhusiano gani na wanawake hao, lakini kwa mujibu wa maandiko, mchunga kondoo wa Bwana anatakiwa kuishi maisha yasiyosababisha maswali ili awe nuru inayomwangazia kila mtu.
Risasi Jumamosi lilimsaka kiongozi huyo wa kiroho ili kutaka kujua kama alikuwa akiogelea kujifurahisha nafsi au kulikuwa na zoezi la kubatiza waumini kama yasemavyo maandiko.
Alipopatikana kwa njia ya simu na kusomewa ‘mashitaka’ yake, askofu huyo aliomba kwa paparazi kuwa, atapiga mwenyewe baadaye kwa sababu alikuwa barabarani akiendesha gari.
“Ndugu yangu nitakupigia baada ya nusu saa, niko barabarani naendesha gari,” alisema mtumishi huyo wa Mungu.
Zilipopita dakika 45 bila kupiga simu kama alivyoahidi, mwandishi wetu alimpandia hewani lakini hakupokea hata pale iliporudiwa mara tano mpaka sita.
Katika habari ya mwanzo ya kunaswa akiwa katika pozi na denti, Askofu Jamal alijitetea kuwa, Basilisa ni binti yake wa kiroho.
Aliongeza kuwa, picha hiyo ya pozi ilipigwa siku akihama nyumba, vitu vikiwa nje yeye alipanda kitandani na kulala ambapo msichana huyo naye alimfuata na kupozi naye.
Alisema aliyepiga picha hizo ni msichana mmoja (hakumtaja) na alimuona akizihamishia kwenye simu ya mwenzake.
Hata hivyo, askofu huyo alisema kuwa, anaamini kuna watu walizisambaza picha hizo kwa lengo la kumchafua, lakini anaamini Mungu atamsafisha.
Habari nje ya chanzo chetu zinaweka wazi kuwa, awali Jamal alikuwa muumini wa imani ya Kiislamu kabla hajachukua uamuzi wa kuwa mkristo na kufikia ngazi ya kuchunga kondoo wa Bwana.
Mara baada ya kuokoka alianza kutoa mahubiri kupitia vituo mbalimbali vya redio nchini akisimulia maisha yake ya nyuma na jinsi alivyokutana na Bwana.

0 comments