Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Maskini Wema, aangua kilio mahakamani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mrembo wa Tanzania mwaka 2006/07, Wema Abraham Sepetu (pichani), amejikuta akimwaga chozi zito mbele za watu huku wengi wakijiuliza kisa ni nini?
Tukio hilo la aina yake lilijiri Mei 18, mwaka huu nje ya Makahama ya Mwanzo, Kinondoni jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kesi yake na Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ kuahirishwa.


Ishu ilianza kama sinema, kwani mara baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Mariam Masamalo kuipiga kalenda, Wema alitoka nje watu wakimkodolea macho. Alikanyaga hatua kadhaa hadi mahali aliposimama Bob Junior na mama yake mzazi (jina halikupatikana).
Kwa mbali, mazungumzo yao hayakuwa yakiashiria kitu chochote, ingawa kuna kipindi mrembo huyo machachari alionekana akinyoosha mikono na vidole kwa familia hiyo kama anayetoa maelekezo fulani.


Ghafla, Wema ambaye alivaa gauni maarufu kwa jina la dela alionekana akilia huku Bob Junior na mama yake wakimwangalia kwa mshangao mkubwa.


Mbaya zaidi, Wema alikinogesha kilio chake kwa kitendo cha kuweka mikono kichwani, wakati mwingine akiziba sura huku akiendelea kuporomosha machozi.
Baadhi ya mashuhuda wasiopitwa na jambo walisogelea eneo la tukio licha ya kwamba, walishindwa kuuliza kilichokuwa kikiendelea.
Baadaye, Wema aliungana na shosti wake mkubwa aliyekuwa amesimama pembeni, Jacqueline Steven Pentzel ‘Jack wa Chuz’ na kuondoka.
Paparazi wetu alimkimbilia Wema kwa nyuma ili kumuuliza kisa cha kumwaga chozi hadharani lakini alishindwa kumfikia mapema, kwani wawili hao waliingia kwenye gari la msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na kuondoka zao.


Paparazi akakaza kifua na kumfuata mama wa Bob Junior (hakutaka jina lake lichorwe gazetini) akamuuliza kulikoni mpaka mlimbwende huyo aangue kilio cha msiba tena nje ya mahakama wakati ‘taito’ yake inamtaka kujisitiri katika mazingira kama yale.
Mama wa Bob Junior: Kusema ukweli mh! Unajua alikuwa amekuja kumwomba mwanangu (Bob Junior) afute kesi. Anasema inamtesa sana.


Mwandishi: Sasa alikuwa analia nini?
Mama wa Bob Junior: Mwanangu amekataa katakata.
Bob Junior alifungua kesi katika mahakama hiyo akimlalamikia Wema kumtukana matusi ya nguoni sanjari na kumtishia maisha.


Kesi hiyo ambayo Wema alikiri kutenda kosa, imesogezwa mbele hadi Juni 9, mwaka huu itakaposikilizwa tena. Aidha, Bob Junior alitakiwa kwenda na mashahidi.
Kabla ya kesi hiyo kutinga kwenye mahakama hiyo, Bob Junior alipeleka mashitaka yake kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam na kufungua jalada la kesi namba OB/RB/6337/2011 MADAI: KUTISHIA MAISHA.


Hata hivyo, hivi karibuni, Wema alisikika kwenye chombo kimoja cha habari cha ‘kielektroniki’ akiwaomba Watanzania wamuombee kufuatia kesi hiyo.
Adiha, alisema amebadilika na kuwa mwananchi mwenye maadili mema huku akilalamikia maisha yake ya nyuma kuwa, yalichangia kumfikisha alipo sasa.

0 comments

Post a Comment