MGOGORO kuhusu mapato katika Kijiji cha Samunge, Liondo umeingia sura mpya baada ya wananchi wa kijiji hicho, kumuondoa madarakani mwenyekiti wao, Michael Lengume, kwa tuhuma za ubadhirifu.Wananchi hao pia wamemteua Mwenyekiti wa Kitongoji cha Samunge, Jonathan Korobei, kukaimu nafasi hiyo.
Lengume aliondolewa madarakani juzi jioni katika mkutano wa hadhara, kufuatia tuhuma za kuingia mkataba wa matumizi ya fedha za mapato ya ushuru wa magari yanayoingia katika kijiji hicho.Inasemekana kuwa kiongozi huyo aliingia mkataba huo na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na kwamba alifanya hivyo bila ridhaa ya wananchi.
Mwenyekiti huyo, pia anatuhumiwa kutotoa taarifa ya matumizi ya Sh27 milioni za ushuru wa magari yaliyoingia Samunge, yakiwapeleka wagonjwa kwa mchungaji Ambilikile Mwasapila.Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya wajumbe wa halmashauri ya kijiji hicho, kupiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti huyo.
Baada ya uamuzi huo, , wananchi walitoa tamko la kutotambua mkataba unaotoza ushuru wa Sh10,000 na kuwaachia Sh4,000 za kijiji kwa magari yanayopeleka wagonjwa.Wananchi hao walidai makubaliano yaliyofikiw na mkutano mkuu yaliafiki kijiji kubakiwa na Sh5,000 kwa ajili ay shughuli ya maendeleo.
Walisema hata hivyo walishangazwa na kitendo cha kuambiwa kuwa fedha zitakazoingia katika serikali ya kijiji zitakuwa ni Sh 4,000 badala ya Sh5,000, hatua ambayo wameipinga.Akisoma tuhuma zinazomkabili Lengume, Mjumbe wa Halmashauri ya kijiji, Steven Lulee, alisema serikali ya kijiji ilikaa na kujiridhisha kuwa mwenyekiti alikuwa hafuatia taratibu.
Alisema pamoja na mambo mengine, kiongozi huyo alishindwa kutekeleza maamuzi ya kijiji."Mwenyekiti amekuwa akijiamulia mambo peke yake bila kushirikisha viongozi kwa hiyo ni mtu ambaye hatufai,"alisema Lulee.
Lulee alisema tuhuma ya tatu ni kuchukuwa Sh1,000,000 kutoka Sekondari ya Samunge na kuifanyia kazi bila kuishirikisha serikali ya kijiji wala kueleza matumizi ya fedha hizo.Mjumbe huyo alifafanua kuwa, Mwenyekiti anatuhumiwa kuchukua Sh13 milioni kutoka benki na hadi sasa hakuna taarifa ya fedha hizo.
Alisema mpaka sasa baadhi ya maeneo ya taasisi yameendelea kuvamiwa bila taarifa zozote, na hivi karibuni Serikali ya kijiji ilipitisha Sh 1,200,000 za vifaa vya ambazo zimetumika bila kutolewa taarifa.Alisema Lengume amegoma kutoa matumizi yaSh 23,071,000 za ushuru wa magari yanayoingia Samunge tangu kuanza kwa zoezi la kukata stakabadhi.
Akichangia hoja katika mkutano huo, Emmanuel Saidea alisema, kiasi cha Sh4,000 zilizoainishiwa kuingia katika Kijiji cha Samunge, zimepangiwa matumizi mengi hatua ambayo inafanya kijiji kisibakie na fedha za maendeleo.
Wakati mkutano huo ukifanyia jana Mwenyekiti Lengume hakuwapo kwa kile alichoeleza kuwa hautambuwi.
Hata hivyo akizungumzia tuhuma hizo jana Lengume alisema maneno yote yaliyosemwa katika mkutano huo ni uzushi na yalipangwa na baadhi ya viongozi ili kutimiza matakwa yao."Hakuna kitu, hawa wanatumiwa tu kutaka kunichafua ili wachache wagawane fedha za ushuru,"alisema Lengume.

0 comments