NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuachia ngazi kwa kuwa tangu amekaa kwenye wizara hiyo, mgao wa umeme umekuwa kitu cha kawaida na kusababisha uchumi wa taifa kuporopoka kwa kasi.
Alisema kuwa waziri huyo amekuwa sasa ni waziri wa mgawo badala ya kuwa waziri ambaye angewasaidia wananchi kuondokana na adha ya umeme unaowawezesha vijana na watu wote kufanya kazi.
"Huyu si waziri na hafai kwa kuwa mgawo kila siku saa 16 kukosa umeme ni hatari kwa makampuni, wafanyabiashara na wananchi kwa jumla,"alisema Zitto na kuongeza:
"Umeme wa mwaka huu kutoka Januari hadi Mei, umeikosesha Serikali kiasi cha Sh850 bilioni. Mwaka 2006 mgawo uliozaa Richmond ulisababisha uchumi kushuka kwa asilimia moja, kitu ambacho ni hatari,"alisema.
Kauli ya Zitto imekuja wakati Tanesco ikiwa umetangaza kuanza kwa mgawo wa umeme ambao ulianza jana na utaendelea kwa wiki kadhaa zijazo. Mgawo huo wa umeme unaelezwa kwamba utakuwa unadumu kwa saa 16 kwa siku na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi.
Alisema kuwa aliposema kuwa Serikali haina fedha hivi karibuni alishambuliwa na viongozi wa Serikali, lakini taarifa yake imewaamsha kwani Serikali na kutaka mishahara iwe inalipwa tarehe 25 ya kila mwezi.
"Nimeambiwa Wizara ya Fedha na Uchumi imewaagiza wakuu wote wa Serikali kuwa ikifika kila tarehe 25 ya mwezi lazima wafanyakazi wawe wamelipwa la sivyo watawajibishwa,"
"Tumekwenda vijijini kabisa ambapo raia wa nchi hii wanaishi pamoja na wakulima ambao ni uti wa mgongo wa taifa, lakini hali zao ni mbaya na Serikali inaendelea kuwakandamiza wananchi hao na hawana pa kusemea,"alisema Zitto.
Mbowe na mauaji Tarime
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alitoa tamko la chama kuhusu mauaji ya Tarime akieleza kuwa haiwezekani polisi wakaendelea kuua raia hivyo wanahamia Tarime mpaka kieleweke.
"Tutahamia Tarime kwa kuwa kwa mujibu wa taarifa ya awali hakuna raia ambaye alipigwa risasi kwa mbele hivyo inaonekana walikuwa wakikimbia hata kama wana makosa wameuawa kikatili,"alisema Mbowe.
Mbowe alisema kuwa hawaendi Tarime kuwatetea wahalifu bali wanakwenda kuwahakikishia haki inatendeka.
Dk Slaa amkaba Membe
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemshangaa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe kwa kueleza kuwa Tanzania ni nchi inayojitegemea na yenye Rais, lakini walipoletewa barua kutoka SFO kuhusu Andrew Chenge, hawakuchukua hatua.
Dk Slaa alisema ni bora hizo fedha ambazo Serikali ya Uingereza inataka kuzitoa kwenye NGO ziende huko kuliko kuzipeleka serikalini kwa kuwa Serikali iliyopo madarakani ni ya kifisadi.
"Ni bora hizo fedha ziende kwa NGO ambayo inaaminika na kuweza kuwasaidia wanyonge,"alisema Dk Slaa.
Alitumia wakati huo kumtaka Ridhiwani Kikwete kwenda mahakamani kwa siku zake alizotoa kwani hana cha kuweza kumsumbua kwa kuwa ni mtoto mdogo.
Alisema kuwa maisha ya wananchi yameendelea kuwa magumu hivyo ni bora Rais Kikwete akae chonjo kutokana na hali hiyo."Juzi nimejiwa na askari polisi wameniambia kuwa usione tunawapiga mabomu, maisha yetu ni magumu,"alisema Dk Slaa.
Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa aliwaambia wananchi wa jimbo hilo kuwa CCM ni meli inayozama, hivyo wawahi mitumbwi Chadema ili waweze kuokoka."CCM njooni Chadema tuwaokoe kutoka katika meli inayozama na msihangaike kupanga viti katika meli inayozama,"alisema Msingwa.Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, alisema kuwa ata
pambana katika bajeti yake ili kuhakikisha maliasili zinawanufaisha wananchi maskini na si viongozi wa CCM waliokalia ufisadi."Nimeagizwa na chama changu kuhakikisha bajeti ijayo tunabanana na Serikali ya CCM ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao,"alisema Msigwa.
Mpendazoe adai Sitta alitaka kuipindua CCM
Kada wa Chadema, Fred Mpendazoe aliendelea kukishambulia CCM kwa kueleza kuwa kimepoteza dira kutokana na kukumbatia na kulinda watu wachache badala ya kupigania watu maskini na wanyonge.
"Ndani ya CCM kuna watu wamejivika ngozi ya kondoo, lakini ni mbwa mwitu wakali, wakina Sitta, Nape Nnauye na Dk Mwakyembe wamekuwa wakijifanya wanawapigania wananchi, lakini ni wanafiki,"alisema.
Alisema kuwa Sitta ndiye aliyetoa samani za ofisi ya CCJ na mpango mzima wa kuipindua CCM, lakini leo bado wapo humo na wanaendelea kuwakandamiza wananchi na kulinda wachache kwa maslahi yao binafsi.
Mpendazoe aliendelea kumkandamiza Sitta kwa kuwaeleza wananchi kuwa aliahidiwa uwaziri baada ya kutemwa uspika na ndiyo maana ameamua kuwasaliti wananchi kwa maslahi yake binafsi.
Hotuba za viongozi hao wa Chadema zilikuja baada ya maandamano makubwa yaliyofanyika jana na kuuteka Mji wa Iringa ambapo wananchi walikusanyika pembezoni mwa barabara wakishangilia huku wengine wakifuatana na viongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho.
Maandamano hayo yalianzia Kihesa hadi Uwanja wa Shule ya Msingi Mlandage na ndiyo yaliyokuwa yakihitimisha operesheni ya Chadema katika mikoa sita kwa muda wa wiki mbili.Operesheni hiyo ya chama hicho iliyoambatana na maandamano katika mikoa hiyo iliweza kupita katika majimbo ya uchaguzi 37 na kuzifikia Kata 224 na vijiji 457 kwa kutumia timu nane ambazo zilikuwa zikiongozwa na viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho.

0 comments