IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MBUNGE wa Viti Maalum (CUF), Magdalena Sakaya na wenzake kumi wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na makosa ya kufanya mkusanyiko usio halali na uchochezi.Sakaya na na wenzake walifikishwa kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Urambo, Oscar Bulugu, baada ya kusomewa mashtaka walikataliwa dhamana.
Mahakama ilielezwa kuwa, baadhi ya majeruhi hali zao siyo nzuri, hali iliyosababisha washtakiwa hao kutopewa dhamana.Hakimu Bulugu alisema shauri la washtakiwa kupewa dhamana au la, litasikilizwa Juni 6, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili itatoa uamuzi wake na watuhumiwa kupelekwa rumande.
Licha ya Sakaya, viongozi wengine wa CUF ni Hashim Bakari, anayetoka Kitengo cha Haki za Binadamu, Yassin Mrutwa, Mjumbe wa Baraza Kuu CUF Taifa, Doyo Hassan, mjumbe wa Baraza Nyanda za Juu Kusini na Kiyungi Amir.
Wanachama wa kawaida waliofikishwa mahakamani, ni Msafiri Alkaida, Hukiny Juma, Singo Yusto, Mrisho Fredrick, Peter Charles na Zainab Seif.Polisi mkoani Tabora imetoa uzito wa shauri, huku viongozi wake wakuu mkoani Tabora nao wamekuwa Urambo kufuatilia, akiwamo Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Liberatus Barlow.
Wakati huohuo, Wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wametua Kijiji cha Usinge, wilayani Urambo, mkoani Tabora kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu kwenye tukio la mapigano lililotokea Mei 28, mwaka huu baina ya polisi na wananchi wa kijiji hicho na kusababisha raia kuuawa.
Wanakijiji walifikia hatua hiyo baada ya Mei 24, mwaka huu polisi hao kukamata ng’ombe 6,301 Kijiji cha Shela, wakidai walikuwa eneo la hifadhi.Kufuatia tukio hilo viongozi wa CUF walikamatwa kwa madai ya kuhusika na tukio hilo; Doyo Hassan, Yasin Mrotwa, Zainab Nyumba na Masoud Omar ambao ni wajumbe wa baraza kuu la chama hicho.
Wengine ni Ofisa wa Haki za Binadamu na Sheria wa chama hicho, Hashim Bakar, aliyekuwa mgombea Ubunge wa chama hicho Jimbo la Urambo Magharibi, Kirungi Kirungi na Sakaya.Mwanasheria wa LHRC, Leticia Petro, alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo, wameamua kwenda kwenye kijiji hicho kujua ukweli.Juhudi za kumpata Kamanda Barlow kwa njia ya simu kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa.
You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Mbunge, viongozi CUF wafikishwa mahakamani
0 comments