Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - CCM kutoa uamuzi sakata la UVCCM, Chatanda

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KATIBU Mwenezi wa CCM mkoani hapa, Loota Sanare amesema uongozi wa chama hicho mkoani unatarajia kutoa uamuzi kamili utakaomaliza utata wa sakata la mvutano baina ya UVCCM na katibu wa chama hicho, Mary Chatanda mwanzoni mwa Juni mwaka huu.


Hatua hiyo inafuatia baada ya zaidi ya vijana 500 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha kuandamana hadi katika Makao Makuu ya ofisi za chama hicho wakimtaka Chatanda andoke kwa madai kuwa amekuwa akikivuruga chama sanjari na kuwachonganisha na viongozi wa dini.


Akizungumza na Mwananchi juzi mjini hapa, Sanare alisema kuwa uongozi wa chama chao kupitia Kikao cha Halmashauri ya Mkoa kinatarajia kukaa mwanzoni mwa Juni ambapo watalitolea uamuzi sakata hilo.


“Sikiliza suala la Chatanda tunatarajia kulitolea uamuzi katika Kikao cha Halmashauri ya Mkoa tunachotarajia kuketi mwanzo wa Juni, hivyo subirini majibu,” alisema Sanare.Hata hivyo, alibanisha ya kuwa mara baada ya vijana hao kuleta malalamiko yao mbele ya chama wao waliwauliza tatizo la katibu huyo ambapo walijibu kuwa moja ya malalamiko ni kitendo kinachofanywa na kiongozi huyo kumkumbatia kada wa UVCCM, Mrisho Gambo.


Alisema kwamba uongozi wa chama mkoa utaangalia kama madai hayo yana msingi au la.Alisema kwa kuwa Chatanda hakuteuliwa na Halmashauri ya Mkoa bali aliletwa na uongozi wa taifa hivyo mara baada ya kikao watapeleka mapendekezo yao juu.


Akizungumzia suala la vijana hao kutishia kuweka kufuli kwenye ofisi ya katibu huyo mwishoni mwa wiki iliyopita, mwenezi huyo alisema kuwa binafsi haamini kama vijana hao wanaweza kufanya kitendo kama hicho kwa kuwa vijana wa CCM ni wasikivu na waadilifu.“Kuhusu suala la kuweka kuful ofisi za katibu wao kwa kweli vijana wetu siamini kama wanaweza kufanya hivyo,”alisema Sanare.


Hivi karibuni kumekuwa na mvutano baina ya UVCCM na Chatanda ambapo vijana hao wametaka katibu huyo aondoke kwa madai ya kukivuruga chama hicho huku Chatanda naye akijibu mapigo kuwa vijana hao hawana mamlaka ya kumng'oa.Vilevile, kuna kundi jingine la vijana wa CCM limeibuka na kuwataka makada wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuachia ngazi mara moja au waondolewe.

0 comments

Post a Comment