Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Wanafunzi wa Udom waandamana, wagoma tena

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), wamegoma kuingia madarasani na kuandamana hadi Ofisi ya Waziri Mkuu mjini hapa, kupeleka malalamiko yao likiwamo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutotimiza ahadi ya kuwapatia kompyuta.

Licha ya mambo mengine, wanafunzi hao wa Chuo cha Teknolojia ya Habari, walisema Pinda aliwaahidi kumnunulia kila mwanafunzi kompyuta ndogo (laptop) kwa ajili ya kumsaidia kwenye masomo yake, lakini hadi jana ilikuwa haijatimizwa.

“Tumeamua kugoma na kuandamana kutokana na ukweli kuwa, matatizo yetu yamekuwa hayapatiwi ufumbuzi tangu mwaka 2007. Menejimenti ya chuo haitaki kutusikiliza na imekula fedha zetu za mahitaji maalum ya kitivo,” alisema Spika wa Bunge la Wanafunzi, Elias Lugwishwa na kuongeza:
“Bodi ya mikopo wanatoa, lakini menejimenti hawataki kutupatia.
Tunasoma sayansi ya kompyuta bila kuwa na kompyuta za kotosha kwa ajili ya mazoezi, hiyo ni elimu au ni uchakachuaji.”
Wanafunzi hao walisema menejimenti ya chuo imekuwa ikitafuna fedha zao za mahitaji maalumu, huku ikitoa vitisho kwa wanaoonekana kuzidai.

Walisema waliamua kuweka wazi kwa menejimenti ya chuo kuwa, watafikisha kilio chao kwa Pinda, ndipo juzi usiku waliambiwa fedha zao zipo tayari na kutakiwa kuangalia majina kwenye mbao za matangazo.
Walisema baada ya kwenda kusoma majina yao, walikuta kiasi kilichoanishwa ni Sh50,000, kiwango ambacho hawakubaliani nacho.

“Siasa, siasa, hatutaki. Tunataka muda maalum wa matatizo yetu yatatatuliwe. Tuhakikishiwe usalama wetu tuwapo chuoni, hatuwezi kutishiwa kila tunapodai haki zetu, wewe mkuu wa wilaya nenda kaongee na manejimenti ya chuo iache kututisha, itusikilize haja zetu,” zilisikika sauti za wanafunzi hao walipokuwa wakiimba.

Hata hivyo, wanafunzi hao hawakufanikiwa kuonana na Pinda, badala yake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Gerald Guninita, aliwatuliza na kuwaeleza kuwa matakwa na matizo yao ameyasikiliza, amewasiliana na Waziri Mkuu kupitia katibu wake na kumweleza kuwa hadi Mei 6, mwaka huu yatakuwa yamefanyiwa kazi.

0 comments

Post a Comment