Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Wakimbizi 700,000 warudishwa Rwanda, DRC

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
ZAIDI ya wakimbizi 700,000 kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) wamerudishwa kwao kuanzia mwaka 2000, huku wengine takriban 100,000 wakitafutiwa makazi ya kudumu nchini.

Wakimbizi hao ni wale ambao walikuwa wamepewa hifadhi nchini kwenye kambi za Nyarugusi na Ntaboba, Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma.  Takwimu hizo ni kuanzia mwaka 2000 hadi sasa.

Akizungumza kwenye warsha ya waandishi wa habari, Ofisa Msaidizi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) nchini, William Ngeze, alisema wakimbizi hao waliorudishwa wengi wao walikuwa mikoa ya Tabora, Kigoma na Tanga.
 “Wakimbizi wengi waliorudishwa ni waimbaji wanakwaya wa Bulyanhulu na wengine kutoka kwenye kambi za Nyarugusi na Ntaboba,” alisema Ngeze.

Ngeze alisema idadi ya wakimbizi hao waliorudishwa inaonyesha jitihada kubwa zilizofanywa na UNHCR na kwamba, waliosalia ambao ni chini ya 100,000 wanatafutiwa eneo la makazi ya kudumu.
Alisema suala la kuwahamisha wakimbizi hao kutoka kwenye kambi hizo na kuwapeleka nyingine, limekuwa gumu kutokana na kukosekana kwa fedha na nchi ambayo iko tayari kuwapokea.

“Ili mtu aweze kuitwa mkimbizi lazima awe na sababu ya msingi iliyomuondoa nchini kwake, ambayo inaweza ikampelekea kukosekana kwa usalama wa maisha yake,” alisema.

Ofisa Mipango Mwandamizi wa UNHCR, Mbogozi Andrew, alisema shirika hilo linatumia dola 22 bilioni za Marekani kila mwaka kuhudumia wakimbizi hao nchini.
Pia, Andrew alisema miongoni mwa huduma wanazozitoa kwa wakimbizi, ni zile za jamii ikiwamo elimu, matibabu, chakula, makazi na malazi.

Alisema wakimbizi wanapokuwa nchini wanatakiwa kufuata sheria kama wananchi wengine na kwamba, iwapo atavunja sheria anahukumiwa kama raia mwingine.

0 comments

Post a Comment