MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepiga marufuku vyombo vyote vya habari kuripoti kesi ya madai ya Sh1, iliyofunguliwa na mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji, dhidi ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, kwa tuhuma za kumkashifu kwa kumtaja kuwa miongoni mwa mafisaidi papa.
Agizo hilo la kwa vyombo vyote vya habari, lilitolewa saa 7:15 mchana wa jana na Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mgeta, wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo hakimu huyo hakusema kama kuna upande wowote katika kesi hiyo,umelalamikia namna vyombo vya habari vinavyoripoti kesi hiyo na wala hakutoa kielelezo chochote kinachoonyesha jinsi vyombo vya habari vinavyokiuka kuripoti mwenendo wa kesi hiyo.
Akitoa agizo hilo, Hakimu Mgeta alisema
"kabla ya kupanga tarehe ya kutajwa kwa kesi hii nina maelekezo na kwamba hakimu atakayeendelea kuisikiliza kesi, mtajua siku hiyo kesi itakapokuja kuendelea kusikilizwa.
"Maelekezo ni kwamba kesi hii imeripotiwa sana na vyombo vya habari ila kinachotupa tabu ni kuripotiwa kwa shahidi kasema nini mahakamani, kaulizwa nini na kajibu nini hivyo taarifa zinapokinzana, zinaathiri uhuru wa hakimu na mahakama kwa jumla,"alisema hakimu Mgeta.
Alisema mahakama ni mahakama ya watu na kwamba kila mtu atakuwa huru kuingia kutazama na kusikiliza mwenendo mzima wa kesi hiyo isipokuwa haitakuwa ruhusa kwa chombo chochote cha habari, yawe magazeti au eletroniki, kuripoti ushahidi wa kesi hiyo.
Kabla ya kutolewa kwa agizo hilo, mmoja wa mawakili wa Manji, Tausi Abdallah, alidai kuwa kesi hiyo ilifikishwa kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mgeta aliiahirisha hadi Juni 3 mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa.
Katika kesi hiyo, Manji anadai fidia ya Sh1 kutoka kwa Mengi kwa madai kuwa amemkashifu kwa kumwita kuwa ni mmoja mafisaidi papa.
Manji pia anaiomba mahakama imwamuru Mengi na Kituo cha Televisheni cha ITV, kurusha kipindi cha kuomba msamaha kwa siku saba, mfululizo kupitia kituo hicho.Mengi anadaiwa kumkashfu Manji Aprili 23 mwaka 2009 katika kipindi maalumu kilichorushwa na ITV baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku.
Katika kesi hiyo, Manji anatetewa na mawakili, Mabere Marando, Richard Rweyongeza, Dk Ringo Tenga na Malima.
Mengi kwa upande wake, anatetewa na mawakili Michael Ngaro, Ringia na Njau.

0 comments