BARAZA la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) mkoani Arusha limesema endapo serikali haitatekeleza mapendekezo ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyotaka kuupatia ufumbuzi mgogoro wa umeya wa Arusha ndani ya siku 21, watafanya maandamano bila kukoma mpaka uchaguzi huo utakapofanyika.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa BAVICHA mkoani hapa, Ephata Nanyaro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa maandamano hayo yatajumuisha vijana kutoka wilaya zote za mkoa wa Arusha.
Alisema kuwa anaupongeza uamuzi huo wa Kamati Kuu ambayo kwa kipindi chote ilikuwa ikiwazuia vijana kuchukua maamuzi wakiwataka wavute subira ili serikali iweze kulitatua ila kwa tamko hilo sasa wamewapa ruksa baada ya Aprili 9 siku hizo 21 zikiisha vijana wako huru kudai haki kwa njia ya amani.
“Ni busara za viongozi wetu ambazo zimefanya hadi sasa umma wa Arusha umekuwa na subira na bado tunaendelea na subira hiyo tukiamini serikali itatumia busara kumaliza utata wa taratibu zilizomuweka meya wa Arusha ndani ya siku 21 vinginevyo tutafanya maandamano bila kikomo mpaka kieleweke,” alisema Nanyaro ambaye pia ni diwani wa kata ya Levelosi kwenye manispaa ya Arusha.
Alisema wao kama vijana wanachopigania ni kuhakikisha nchi inaongozwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, haki na usawa jambo alilodai kuwa ndilo linalowasukuma kuandamana kuishinikiza serikali kuhakikisha uchaguzi wa meya Arusha unafanyika kwa mujibu wa sheria.
Alisema kuwa watafuata sheria na taratibu zote za kuandaa maandamano ikiwemo kutoa taarifa polisi ambapo vijana wote wataandamana kuelekea kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Arusha watakakokutanika na kuweka kambi hapo mpaka.
serikali itakapoamua uchaguzi huo ufanyike akiweka wazi kuwa wamejiandaa kisaikolojia kukumbana na vitisho na matumizi yoyote ya nguvu dhidi yao.
Nanyaro alibainisha kuwa wanachotaka wao si CHADEMA kushinda umeya bali meya apatikane kutokana na taratibu halali za kisheria ili kujengeke desturi ya sheria na taratibu kuheshimiwa badala ya ubabe wa CCM kuwa ndio sheria.
Awali Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa msimamo wa chama hicho uliofikiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu iliyokutana jijini Dar es Salaam Machi 19, mwaka huu, akitoa siku 21 kwa serikali kuupatia ufumbuzi mgogoro wa umeya wa jiji la Arusha.
Mbowe alisema kuwa CHADEMA ilipuuza maelezo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyewataka wasioridhika na uchaguzi wa meya waende mahakamani akisema endapo wangeenda mahakamani ni sawa na kukubali kwamba uchaguzi ulifanyika, jambo ambalo linajenga msingi wa CCM kung’ang’ania madaraka popote inaposhindwa, huku ikidhani wananchi watakiachia tu na kukimbilia mahakamani.
Kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni alisema baada ya siku 21 chama hicho kitaamua la kufanya, kama njia ya kurejesha majibu kwa wananchi wa Arusha ambao wamekuwa wakidai majibu na hata kutaka kuchukua hatua ambazo viongozi wa CHADEMA wamekuwa wanazuia.
Vile vile, alipuuza hoja ya Pinda aliyesema kwamba kwa idadi ya madiwani 16 wa CCM, 14 wa CHADEMA na mmoja wa TLP, ilikuwa wazi CCM kingeibuka mshindi.
Mbowe alihoji kama wingi wa madiwani ni hoja, ilikuwaje TLP yenye diwani mmoja ikapigiwa kura na madiwani 16 wa CCM; na akatoa mfano wa Halmashauri ya Hai ambako CCM kina madiwani wengi lakini mwenyekiti wa halmashauri aliyechaguliwa kwa kura nyingi ni wa CHADEMA.
Januari 5 mwaka huu CHADEMA walifanya maandamano kupinga taratibu zilizotumika kumpata Meya wa Arusha, Gaudence Lyimo, ambapo jumla ya watu watatu walifariki kwa kupigwa risasi na polisi huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya.

0 comments