WABUNGE wa Kamati ya Hesabu za Serikali, wamehoji matengenezo ya helkopta moja ya jeshi la Polisi kugharimu zaidi ya Sh 1,189,790,560 (dola za Marekani 849,850.4).
Mbali ya kiasi hicho kikubwa cha fedha, wabunge hao wamehoji pia hasara ya zaidi ya Sh 560milioni (dola 400,000) iliyotokana na kucheleweshwa kulipwa kwa gharama za awali za matengenezo ya helkopta hiyo ambazoawali, zilikadiriwa kuwa Sh 774,178,342 (dola 552,984.53).
Helkopta hiyo aina ya Bell 206L namba 5H-PAW, ilipelekwa Afrika Kusini kwa matengenezo, miaka miwili iliyopita ikiwa ni miaka minne tangu iliponunuliwa mwaka 2006.
Wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zainab Vullu, Wabunge Stephen Masele (Shinyanga Mjini) na Ali Mohamed Kessy (Nkasi Kaskazini), walikuwa mstari wa mbele kuwabana polisi ambao katika kikao hicho, waliongozwa na Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta Jenerali Said Mwema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Walikuwa wakijadili taarifa ya ukaguzi wa fedha za jeshi hilo za mwaka ulioishia Juni 30, 2009.
Hata hivyo, taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zinaonyesha kuwa hakuna uhakika kama matengenezo husika, yamefanyika kwa kuwa hakuna taarifa za kiufundi za kuthibitisha hilo wala uhalali wa kufanyika malipo hayo.
Mhasibu wa Jeshi hilo, Frank Msaki alisema kuwa hati ya kuthibitisha matengenezo ya helkopta hiyo, itapatikana baada ya kukamilika kwa matengenezo na kwamba kuchelewa kukamilika kunatokana na uhaba wa fedha. Alisema juhudi za kupata fedha hizo kutoka Hazina zinaendelea.
Wabunge hao walisema fedha zinazotumika kwa matengenezo ya helkopta hiyo ni nyingi na kushauri iuzwe na kununuliwa helkopta nyingine.
Kamishna wa Polisi, Coldwig Tweve alisema polisi ilituma ombi maalumu la fedha Hazina, ili kulipa madeni yake pamoja na deni hilo la helkopta lakini hawajajibiwa.
Alisema helkopta hiyo ilinunuliwa mwaka 2006 kwa Sh5 bilioni na kwambab hivi sasa bei ya helkopta mpya ya aina hiyo imefikia Sh8.49 bilioni.
Hata hivyo, taarifa ya CAG inaonyesha kuwa kati ya mwaka 2005/2006, polisi ilifanya matumizi ya ziada ya Sh284,265,206 bila ruhusa ikiwamo kufanya manunuzi ya Sh253,603,293. |Msaki alisema walipeleka ombi maalumu Hazina ili waruhusiwe kutumia pesa hizo pamoja na kufanya manunuzi hayo. Polisi inadaiwa zaidi ya Sh26.5 bilioni na askari wake pamoja na wazabuni.
Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Ramadhani Hamisi alisema Hazina itawasilisha katika kikao kijacho cha Bunge, hati ya matumizi hayo ya dharura.
Inspekta Jenerali Mwema alisema helkopta hiyo ilinunuliwa ili kusaidia utendaji wa kazi za jeshi hilo na kwamba kuharibika kwake kunakwaza utendaji wao wa kazi.

0 comments