WAKAZI wa Dodoma wameha- kikishiwa maji ya uhakika mara baada ya kukamilika kwa mradi wa kuongeza uzalishaji unaofadhiliwa na Serikali ya Korea ya Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka mjini Dodoma (Duwasa), Peter Mokiwa alisema Serikali ya Korea ya Kusini imekubali kuikopesha Tanzania dola milioni 49.6 za utekelezaji wa maradi huo.
"Lengo ni kuongeza uzalishaji na kufikia meta za ujazo 61,500 kwa siku badala ya meta za ujazo 30,000 zinazozalishwa sasa," alisema.
Mokiwa alisema shughuli nyingine za mradi huo ni ujenzi wa mitandao ya kusafirisha maji kutoka visimani na ujenzi wa bomba jipya lenye kipenyo cha milimeta 600 litakalosafirisha maji kutoka Mzakwe yanakazolishwa maji hayo hadi mjini.
Alisema kukamilika kwa mradi huo kutakuwa mkombozi kwa wakazi wa Dodoma kwa kuwa kutaondoa upungufu wa maji na kufikisha maji maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema mara baada ya kupatiwa mkopo huo, mradi huo utaanza na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha mwaka mmoja hadi miaka mitatu.
Mji wa Dodoma una mahitaji halisi ya meta za ujazo 54,000 wakati uwezo wa kusafirisha maji kuja mjini ni meta za ujazo 30,000 tu.

0 comments