Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Msaidizi wa Rais aikana tume ya maadili

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MSAIDIZI wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya siasa, Bw. Rajab Luhwavi amekana mbele ya Baraza la Maadili kwamba hajawahi kupewa fomu kwa ajili ya kutoa
tamko rasmi juu ya mali zake kutoka sekritarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

Akizungumza katika kikao kilichoandaliwa na baraza hilo Dar es Salaam jana, Bw. Luhwavi alisema baada ya kuteuliwa kushika  nafasi hiyo mwaka 2006 alikwenda katika sekritarieti hiyo kuomba fomu lakini aliambiwa asubiri barua ya wito.

Alisema alidhani hayumo kwenye orodha ya watu wanaotakiwa kutoa matamko juu ya mali wanazomiliki kwa sababu tangu apewe jibu hilo alikaa muda mrefu bila kupata barua ya wito wala fomu.

Alisema mwaka 2008 sekretarieti hiyo ilimtumia barua ya wito na siyo fomu ambayo haikuonesha tarehe anayotakiwa kuripoti.

Hata hivyo ,aliwataka viongozi wa sekritarieti hiyo kutumia utaratibu ambao utasaidia barua hizo kuwafikia wahusika kwa wakati ili kupunguza malalamiko yanayojojitokeza kila mara.
 
Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala ambaye pia aliitwa mbele ya bara hilo akidaiwa kuwa anaidanganya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa sababu fomu zake zinaonesha zilipelekwa Agosti 2010 wakati yeye anasema zilipelekwa Januari 2010.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Baraza la maadili Jaji Mstaafu Bw. Damiani Lubuva aliwataka viongozi wa umma kutambua wajibu wao wa kutoa matamko kila mwisho wa mwaka juu ya madeni na mali wanazomiliki na siyo kuisubiri sekritarieti kuwatumia barua za kuwakumbusha.

Pia alisema viongozi wa umma watambue kwamba utawala bora na wa kidemokrasia unapatikana pale wanapozingatia suala zima la maadili.

"Kutoa matamko juu mali za wanazomiliki ni sheria ambayo ipo na inatambuliwa na kila kiongozi wa umma," alisema.

Alisisitiza kuwa sekritarieti itaendelea kuwapelekea fomu lakini nao wajitahidi kujiwajibisha.

Alizitaka taasisi zinazohusika kuhakisha barua zinawafikia wahusika na kuzirudisha kwa sekritarieti hiyo kwa wakati.

Pia aliwataka viongozi wa umma kuwa makini na matapeli ambao wanaoitumia sekritarieti hiyo kuwaambia kwamba wamo kwenye orodha ya wanaotakiwa kutoa matamko juu ya mali zao.  

Alisema katika vikao vilivyofanywa na baraza hilo tangu Aprili 11 hadi 18 mwaka huu wamezungumzia suala la matamko juu ya mali lakini katika vikao vingine watajadili kama kuna ukweli juu ya mali walizoandikisha.

Alisema kinachofuata ni baraza hilo kuyafanyia kazi yote yalizungumzwa na baadaye mapendekezo yatatolewa.

Jaji Lubuva alisema wamepata ushirikano mkubwa kutoka kwa viongozi wote walioitwa katika sekretarieti hiyo.

0 comments

Post a Comment