Basi la Ngorika likiwa limepinduka |
Harakati za kumtoa dereva wa Basi la Ngorika, Emanuel Mchoro(30) lakini kwa bahati mbaya alikuwa keshakufa, baada ya kulaliwa na basi hilo kwa muda wa masaa matano. |
Gari Dogo aina ya Toyota Hiace likiwa halitamaniki baada ya kugongana na Basi la Ngorika mapema leo asubuhi. |
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Arusha,Thobias Andengenye, alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 12:30 asubuhi katika eneo la Makumira nje kidogo ya mji wa Arusha.
Alisema kuwa ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota hiece lenye namba za usajili T 773 BGT lililokuwa likiendeshwa na Selemani Juma (30)mkazi wa kijenge na Basi la Ngorika aina ya Scania lenye namba T 633 ANF lililokuwa likiendeshwa na Emanuel Mchoro(30) mkazi wa Mwanga kilimanjaro.
Kamanda Andengenye alisema kwamba chanzo cha ajali hilo kimetokana na gari aina ya haice kutaka kulipita gari lililokuwa mbale yake akiwemo mwendesha baiskeli ,hata hivyo kabla ya kufikia uamuzi huo aliona basi hilo la Ngorika likija kwa kasi na ndipo alipoamua kuingia porini ili kujinusuru asigongane uso kwa uso.
Hata vivyo kabla dereva huyo wa haice hajafika mbali ndipo gari hilo la ngorika lilimgonga ubavuni na kusababisha watu 9 waliokuwa ndani ya gari hiyo kufariki dunia papo hapo.
Andengenye aliwataja marehemu hao kuwa ni, Kizo Rafael Ndosi (35) mkazi wa Arumeru,Patriki Temba (28) mkazi wa Usariver,Samsoni Emanuel Minja (60),Hamisi Charles(30) mkazi usar river,John Kess(38) mkazi wa majichai,Huruma Safiel (28)mkazi wa usar river,Emanuel Mchoro (30) mkazi wa mwanga ambaye yeye ni dereva wa gari ya ngorika.
Mungine ni Fatuma Msuya (35)mkazi wa usar river ambaye yeye ndiye mwanamke pekee aliyekukfa katika ajali hiyo pamoja na dereva wa baiskeli aliyejulikana kwa jina moja la Elvisa.
0 comments