Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Azzan atoa siku kumi Sekretarieti kujiuzulu.

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MBUNGE wa Kinondoni, Iddi Azzan

MBUNGE wa Kinondoni, Iddi Azzan, ametoa siku kumi kwa Sekretarieti ya CCM na Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es Salaam, kujivua gamba ili kukinusuru chama na hali mbaya ya kisiasa iliyopo.
Azzan alisema iwapo viongozi hao hawatajiuzulu kwa muda huo, ataitisha mkutano wa vyombo vya habari na kueleza maovu yote waliyofanya wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu mwaka jana.
Katika muda huo, Azzan alisema anataka viongozi hao kuitisha mkutano utakaojadili tathmini ya uchaguzi wa mwaka jana, utaratibu ambao unatakiwa kufanywa kwa mujibu wa mwongozo wa CCM.
Akizungumza ofisini kwake Kinondoni, Dar es Salaam juzi, Azzan alisema viongozi hao wanatakiwa kutambua kuwa, CCM sio chama cha mtu mmoja, bali cha jamii ya Watanzania, hivyo kila kiongozi anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa kanuni na taratibu zilizowekwa.
Mbunge huyo alisema tangu Novemba mwaka jana, aliwataka viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, kuitisha mkutano wa kujadili tathmini ya uchaguzi huo.
Alisema viongozi hao wamekuwa wakikwepa kuwajibika kwa kutoa majibu ya kubabaisha, kama yaliyopita si ndwele na asitafutwe mchawi.



"Nimepokea simu tatu zinazoniambia kwamba ninyamaze, vinginevyo nitakiona cha moto, nyingine ikaniambia nitanyang'anywa kadi ya uanachama wa CCM, nasema katika kutetea haki na utaratibu stahili wa CCM nitasema ukweli sitamwogopa fisadi yoyote na nimetoa siku kumi wajivue gamba vinginevyo ama zangu au zao," alisema Azzan.
Awali, Mbunge huyo akiwa Dodoma bungeni wiki iliyopita alitoa wito kama huo, lakini Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng’enda, alikataa kwamba hatajiuzulu.
Hata hivyo, taarifa ambazo zimevuja kutoka kwenye ripoti ya tathmini ya uchaguzi uliopita ambayo ilitumika kuong’oa Sekretarieti ya CCM taifa, inadaiwa inapendekeza katibu huyo kufukuzwa.
Azzan alisema Dar es Salaam ilifanya vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka jana na kwamba, hali iliyosababisha majimbo mawili na madiwani wa kata 17 kuangukia mikononi mwa wapinzani.
Alisema hali hiyo sio kwamba wananchi hawaitaki CCM, bali wagombea waliowataka hawakurejeshwa na viongozi kutokana na fitina, hadi kufikia sekretarieti kuanza kuwaandama wagombea wa chama kama yeye aliyeonyesha msimamo.



0 comments

Post a Comment