UMOJA wa vijana wa CCM Mkoa wa Tabora, umemuondoa kwenye nafasi ya ulezi wa jumuiya hiyo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga, alisema uamuzi huo umefikiwa kufuatia matamshi aliyotoa mlezi huyo kwa gazeti hili jana kuwa UVCCM wana matatizo.Kamoga alisema kikao kilichofanyika Mjini Dodoma cha UVCCM kilitoa maazimio ambayo yalikuwa ni ya wajumbe wote, ukiwamo Mkoa wa Tabora ambao Sitta ni mlezi wa mkoa.
Alisema Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, angeona kuna tatizo angewaita na kuwaeleza walikopotoka sio kuchukua uamuzi wa kuzungumza kupitia chombo cha habari.
"Kama mheshimiwa Sitta angeona kuna tatizo katika maazimio yao angetuita sisi kama vijana wake na yeye akiwa mlezi wetu angetueleza mahali tulikopotoka," alisema.Alipoulizwa kama tayari wamemtaarifu kuhusu uamuzi huo, Kamoga alisema hawana sababu ya kumtaarifu kwa barua, kwani hata wao hawakumteua kwa jinsi hiyo.
Kuhusu kama kuna kikao chochote kilichoketi kuchukua uamuzi huo, mwenyekiti huyo alijibu kuwa suala hilo halihitaji vikao, bali tamko la mwenyekiti linatosha.Alibainisha kwamba hata uteuzi wa mlezi hufanywa na mwenyekiti na vikao humpitisha na kwamba, yeye alimkuta Sitta akiwa mlezi wa UVCCM na waliendelea naye.
Alisema iwapo hatua ya kumuondoa isingechukuliwa, vijana na watu wangewashangaa kufuatia matamshi aliyoyatoa.Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa, alipozungumza na Mwananchi, alikiri kupata taarifa kutoka Mkoa wa Tabora.
Alisema wao kama viongozi wa kitaifa hawana pingamizi na uamuzi uliofikiwa, kwa sababu uamuzi wa mkoa hawawezi kuuingilia.

0 comments