MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imerejesha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jalada la kesi ya madai ya fidia ya Sh1, inayomkabili Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi na kuagiza kesi hiyo iendelee kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana.
Jalada hilo lilitishwa katika mahakama kuu na Jaji Mfawidhi, Semistocles Kaijage, kufuatia ombi la Mengi kupitia kwa wakili wake, Michael Ngalo.
Katika ombi hilo, Mengi alilalamikia kile alichodai kuwa ni kutokuridhishwa na namna hakimu Aloyce Katemana, anavyondesha kesi hiyo.Malalamiko hayo yalikufuatia tukio la Februari 11 mwaka huu, wakati haki huyo, alipozikataa nyaraka 14 zilizowasilisha na Mengi ili ziwe sehemu ya vielelezo vya ushahidi katika utetezi wake.
Februari 23 mwaka huu, wakili wa Mengi, Ngalo alindika barua kwenda Mahakama Kuu ya Tanzania, akilalamikia jinsi hakimu Katemana anavyoiendesha kesi hiyo.Alidai kuwa hakimu huyo alikuwa analia upande mmoja na kwamba hata uamuzi wake ulikuwa wa mashaka.
Wakili huyo alimuomba Jaji Kaijage, alipitie jalada la kesi hiyo.Hata hivyo habari zilizopatikana jana zilisema baada ya kupitia jalada hilo, Jaji Kaijage, aliridhika kuwa hakuna ukiukwaji wa sheria wala taratibu katika uendeshaji wa kesi hiyo na hivyo kuagiza jalada lirejeshwe katika Mahakama ya Kisutu, ili kesi iendelee kusikilizwa mbele ya hakimu Katemana.
Pamoja na kurejesha jalada hilo, jaji Kaijage pia alimtaka wakili Ngalo kama atakuwa , awasilishe ombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ombi la kutaka hakimu huyo ajitoe kusikiliza kesi hiyo.
Habari zilisema tayari jalada hilo limekwisha rejeshwa katika Mahakama ya Kisutu, tangu juzi.
Awali, Hakimu Katemana alitupitilia mbali ombi la Mengi kupitia wakili wake , la kutaka kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Februari 11 mwaka huu, kwa sababu sheria hairuhusu panapotokea ubishi mdogo wa kesheria na ambao hauwezi kumaliza kesi, kukatiwa rufaa au kufanyiwa mapitio.
Awali Februari 11, mwaka huu, Katemana alitoa uamuzi Katika kesi hiyo ya madai ya Sh1 iliyofunguliwa na Manji dhidi ya Mengi na zilizotupiliwa mbali, nyaraka 14 zilizowasilishwa na Mengi kwa madai kuwa hazina msingi.
Nyaraka hizo ni pamoja na mkataba kuhusu kampuni ya Quality Finance Cooparation Group na Kagoda Agriculture.Nyaraka hizo za Mengi zilitupiliwa mbali mahakamani hapo kwa sababu zilikuwa hazina kibali kutoka kwa ofisa wa serikali na kwamba hazimuhusu Manji.
Uamuzi huo ulikuja baada ya Wakili wa Manji, Mabere Marando,kuiomba mahakama ya kufuta nyaraka zilizowasilishwa na Mengi kwa maelezo kuwa zinapingana na matakwa ya kisheria.Marando alidai kuwa sheria inakataa nakala zisizo halisi, lakini ipo sheria ambayo inaruhusu kuomba kibali ambacho ilitakiwa upande wa Mengi wakipeleke kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.
"Na kama waraka unahusu serikali unatakiwa ufanyiwe marekebisho na ofisa aliyetoa nyaraka hizo na kwamba inatakiwa zilipiwe,lakini upande wa Mengi vitu hivyo vyote havijafanyika,"alidai Marando.
Aliongeza kudai kuwa kutokana na hoja hizo,nyaraka zote zilizopelekwa mahakamani hapo na upande wa Mengi hazina msingi na zinapaswa kuondolewa mahakamani.

0 comments