RIPOTI za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, zilizowasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete, zimebainisha kuwa bado kuna mapungufu na changamoto nyingi zinazohitaji kurekebishwa.
Mkaguzi mkuu katika ripoti hizo, ametoa mapendekezo muhimu yanayolenga katika kudhibiti matumizi ya fedha na rasilimali za nchi,mapendekezo ambayo rais ameyaafiki.
Kufuatia kuafiki huko, Rais Kikwete amemtaka Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha, kuwasilisha bungeni ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Serikali, kwa Hesebu za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Ukaguzi wa Ufanisi kwa mwaka 2009/0.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kurugenzi ya Mawasiuliano Ikulu, ripoti hizo zinatakiwa kuwasilishwa bungeni, Aprili 12 mwaka huu.
Ilisema tayari mkaguzi mkuu alikwishawasilisha ripoti hizo kwa rais juzi, kulingana na matakwa ya katiba iliyorekebishwa mwaka 2005, kifungu cha 28 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma namba 11 ya mwaka 2008.
Kwa mujibu wa sheria, ripoti hizo zinapaswa kuwakilishwa kwa rais kabla ya tarehe ya mwisho ya mkutano wa Machi na kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuwaandikia mawaziri wanaohusika,ili waweze kuwasilisha kwenye kikao cha Bunge linalofuata.

0 comments