Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Dewji ataka Phiri asimamishwe Simba

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MWANACHAMA wa klabu ya Simba, Azim Dewji ameitaka  klabu hiyo kutouvumilia utovu wa nidhamu unaofanywa na kocha wao mkuu Patrick Phiri na badala yake amependekeza asimamishwe.

Dewji, mfadhili wa zamani wa klabu hiyo aliyeifikisha fainali za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka 1993, ilipotolewa na Stella Abidjan ya Ivory Coast alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumzia uwezekano wa klabu yake kuitoa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

Klabu hizo zinakutana mwishoni mwa wiki katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa na katika mchezo wa kwanza, Simba iliteleza kwa kufungwa mabao 3-1, lakini sasa ikijiandaa kujibu mapigo katika mchezo wa marudiano mwishoni mwa wiki hii.

Alisema: “Nilikuwa kule Lumbumbushi kuiongezea nguvu, tulifungwa, lakini Mazembe wanaweza kufungika. Lakini, kwa staili hii ya kocha Phiri (Patrick) mtafanyaje vizuri?

“Kule niliona mapungufu kadhaa kama ilivyokuwa kwa viongozi, wachezaji na mashabiki  wa Simba wengine. Kama kocha angeendelea na programu yake kwa wakati, timu ingekuwa imeshakaa sawa, lakini angalia, kocha bado yuko kwao Zambia wakati timu iko vitani, tena na wazoefu kama Mazembe, inashangaza sana!”

Dewji aliongeza kuwa kwa kocha anayeipenda kazi yake, kamwe asingethubutu kuitelekeza timu kwa karibu wiki moja katika kipindi cha maandalizi ya mchezo muhimu wa marudiano dhidi ya Mazembe.

“Nakuambia, kwa kocha anayeipenda kazi yake, siku mbili alizopewa zingemtosha na kurejea, lakini amejiongezea siku hadi wiki. Katika suala la nidhamu, wachezaji wajifunze nini kutoka kwake?

“Naushauri uongozi kwamba ili kuweka nidhamu ndani ya klabu, akirejea Phiri asimamishwe hadi baada ya mechi na Mazembe. Angekuwa na uchungu angekuwa na timu kuipika zaidi na zaidi, lakini hajaonyesha kujali zaidi ya kuwapiga danadana viongozi,” alisisitiza Dewji.

Baada ya kuteleza  kule DRC, Simba inatakiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo ujao Jumamosi ili iendeleze rekodi ya kuwavua ubingwa wafalme wa soka Afrika, kama ilivyokuwa kwa Zamalek ya Misri mwaka 2003.
Tags:

0 comments

Post a Comment