BAADA ya serikali kuhofu kununua mitambo ya Dowans, Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) huenda likanunua mitambo hiyo.Uamuzi huo wa CTI kununua mitambo hiyo iliyoibua jinamizi la Kampuni ya Richmond, unatokana na dhamira yake iliyoitoa ndani ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, hivi karibuni.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo January Makamba, alisema kumekuwa na mazungumzo kati ya pande zinazohusika kuhusu ununuzi wa mitambo hiyo.Kwa mujibu wa Makamba, hatua hiyo imekuja baada ya serikali kupata kigugumizi katika kununua mitambo hiyo.
Alisema kwa msingi huo, huenda sasa mitambo hiyo ikauzwa kwa CTI, ili isaidie katika kuondoa tatizo la mgawo wa umeme nchini."Watu wa serikali wamekosa ujasiri katika kufanya maamuzi magumu ya kununua mitambo ya Dowans. Lakini, sasa hivi jopo la wenye viwanda linafikiria kuinunua," alisema.
Makamba alisema katika kikao kati ya kamati na CTI, liliibuka wazo la kuhusu wenye viwanda kununua mitambo hiyo.Mwenyekiti huyo wa kamati yenye dhamana ya nishati nchini, alisema "mitambo hiyo ikiwashwa siyo tu itainufaisha CTI au kupunguza mgawo kwenye viwanda tu, bali hata kwa wananchi na maeneo mengine."
Alisema mazungumzo kuhusu suala hilo yanahitaji kushirikisha pande nyingi kwani yatapaswa kuonyesha mkataba ambao CTI itauza umeme kwa Tanesco.
"Itabidi Ewura (Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji) iridhie, bodi ya Tanesco wenyewe na upande mwingine wa serikali," alifafanua.Hata hivyo, alirejea msimamo wa kamati akisema kinachohitajika sasa ni nchi kuondokana na mgawo wa umeme kwa kuwashwa mitambo yote muhimu na si vinginevyo.
"Watu wanahofu kununua mitambo ya Dowans kwa sababu za kisiasa. Wengine wanahoji tukiinunua itakuaje lakini hili si jambo la siasa." alisema Makamba"...basi kama hawataki Dowans serikali ipeleke pesa za kutosha kwa IPTL, ili wakazalishe umeme wa kutosha na nchi iondoke hapa ilipo," alisisitiza
Makamba alisema kwa hali ilivyo sasa, hata mpango mkakati wa Kilimo Kwanza, hautaweza kufanikiwa kutokana na tatizo la mgawo wa umeme ambao hugusa sekta mbalimbali ikiwemo uzalishaji mbolea kama katika kiwanda cha Minjingu.
Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa CTI Hussein Kamote, alipoulizwa alikiri kuwepo kwa mazungumzo lakini alisema "siyo mimi ninayeshughulikia suala hilo. Ni mwenyekiti wangu mzee Mosha (Felix) na Mkurugenzi Mtendaji (Christina Kilindu)."

0 comments