Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mlimani waanzisha shahada mpya mbili

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, kimeanzisha Shahada ya Juu ya Biashahara za Kimataifa na Shahada ya Biashara na Masoko ya Kimataifa. Shahada hizo zilizunduliwa jana na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu, katika hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo.Katika hotuba yake, Naibu waziri alikitaka chuo hicho kiendelee kuwa mfano wa kuigwa na vyuo vingine hapa nchini.Pia alivitaka vyuo hivyo vingine, kupata uzoefu kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

"Vyuo vingine vitaendelea kupata uzoefu kutoka katika chuo hiki ambacho ni chuo mama hapa nchini na Afrika Mashariki. Kitendo cha kuanzisha shahada hizi, kitakifanya chuo, kiendelee kuaminika kimataifa,"alisema Nyalandu.
Alisema kwa sasa chuo hicho kinajipanga ili kuanzisha vituo ambavyo wanafunzi watavitumia katika kupata mafunzo ya shahada hizo za biashara.Kwa mujibu wa waziri, mafunzo hayo yatawawezesha wahitimu kuwa na uwezo wa kuajiriwa katika sehemu yoyote ya ndani na nje ya nchi.

Nyalandu aliishauri serikali na kampuni binafsi, kutoa kipaumbele cha ajira kwa wataalamu watakaokuwa wanahitimu fani hizo."Sekta ya umma na sekta binafsi, hazinabudi kutoa kipaumbele kwa Watanzania watakaomaliza masomo hayo ili kuwapa moyo wa kuona kuwa wanathaminiwa, kuliko wageni wakati," alisema Naibu waziri.

Mshauri wa Wanafunzi katika kitivo hicho, Dk Marcellina Chijoriga, alisema kuanzishwa kwa shahada hizo, kumekuja baada ya kuona kuwa wanafunzi wanaomaliza masomo ya biashara, hawafanyi vizuri katika shughuli za kibiashara na masoko.Alielezea matumaini yake kuwa kuanzishwa shahada hizo kutawawezesha watu wengi kuingia katika soko la ushindani.
Tags:

0 comments

Post a Comment