WAKATI Serikali ikipiga marufuku michango holela katika shule zake nchini, uongozi wa shule ya msingi Amani iliyopo Buza, Temeke unadaiwa kuchangisha zaidi ya Sh milioni 264 kwa mwaka, kutoka kwa wanafunzi wake, kinyume cha sheria.
Fedha hizo zinazodaiwa kuwa ni posho ya walimu kwa ajili ya kufundisha masomo ya ziada na tozo la mitihani ya majaribio ya kila mwisho wa wiki huanzia Sh 300 – Sh 700 kwa kila mwanafunzi.
Aidha, kwa kila mwezi, shule hiyo inakadiriwa kukusanya Sh milioni 26.4 ambapo kwa muda wa miezi 10 ya masomo, kila mwanafunzi hulazimika kulipa Sh 88,000 gharama za huduma hiyo.
Wakizungumza na gazeti hili Dar es Salaam juzi, baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo, walisema wanafunzi wanaoshindwa kulipa fedha hizo hubaki kuwa watazamaji wakati wenzao wakifanya mitihani au kurudishwa nyumbani.
Walisema kwa mwaka wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza hulazimika kulipa jumla ya Sh 175,000 za madawati, posho ya walimu na kompyuta.
“Ikiwa Serikali ilitangaza kuwa elimu ni bure kwa nini sisi tunalipia kiasi hicho kama shule za kimataifa?
Na wanafunzi wanatozwa fedha za kompyuta wakati hata umeme hakuna na isitoshe imeshazoeleka, kuwa mtoto asiposoma tuisheni katika shule ya Amani, matumaini ya kufaulu darasa la saba huwa finyu,” mmoja wa wazazi ambaye hakupenda kuandikwa gazetini alisema.
Aliongeza kuwa kutokana na maslahi hayo, walimu wa shule hiyo wametilia mkazo masomo ya ziada zaidi kuliko ya kawaida darasani, hali inayowakandamiza wanafunzi wasio na uwezo wa kumudu gharama hizo.
“Sisi wazazi wenye hali ya chini ambao wakati mwingine tunashindwa kumudu gharama hizo tumeshajizoelea kuwa, Ijumaa watoto wetu wanakuja shuleni kucheza kwa sababu ni maalumu kwa waliolipia mitihani,” aliongeza.
Gazeti hili lilihudhuria kikao cha wazazi na uongozi wa shule hiyo, ambapo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Geofrey Chipanda, aliwataka wazazi hao kutoogopa gharama, kwani fedha hizo hutumika kama motisha kwa walimu ya kuwasaidia wanafunzi waongeze ufaulu wa shule hiyo.
“Kumpa motisha mwalimu si kazi ya Serikali bali ni ninyi wazazi na kwa sasa tumeanzisha utaratibu mpya wa malipo ya gharama za masomo ya ziada hatutaki kupokea Sh 300 kwa siku, kama ilivyokuwa awali bali tunataka itolewe kwa awamu,” alisema Chipanda.
Chipanda aliendelea kufafanua:“Namaanisha kwa malipo ya wiki mbili yatakuwa Sh 3,000 na kwa mwezi Sh 6,000 au kama mzazi ataweza kumudu ni vizuri akalipia miezi 10 kabisa Sh 60,000 na ukijumlisha na mitihani ya kila wiki ambayo ni Sh 28,000 inafikia Sh 88,000,” alisema Chipanda.
Alisema walimu wa shule hiyo wamekuwa wakifundisha wanafunzi kwa awamu tatu; kuanzia saa 12.30 hadi saa 1.30 asubuhi hufundisha waliolipia gharama hizo na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana hufundisha wote na saa 9.30 alasiri hadi saa 12 jioni huendelea na waliolipa.
Alisema michango mingine ni ya kawaida, kwani hulipwa kwa wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza, ikiwa ni pamoja na gharama za kutengeneza madawati na kubainisha kuwa ada ya masomo ya ziada ni makubaliano kati ya wazazi na walimu, ili kutafuta ushindani wa kitaaluma na shule za kimataifa.
Gazeti hili pia lilizungumza na Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba, ambaye alisema hana taarifa hizo na kubainisha kuwa utaratibu waliojiwekea na walimu wake, ni kusaidia wanafunzi wenye uelewa mdogo kiakili kwa kuwafundisha masomo ya ziada bila kuchangia fedha yoyote.
“Kutokana na mlundikano mkubwa wa wanafunzi madarasani, wengine wanakuwa hawaelewi, hivyo kwa kukabiliana na hali hiyo, tulikaa na walimu wa shule zetu zote na kukubaliana kuwasaidia kwa kuwafundisha masomo ya ziada ili kuongeza ufaulu wa mitihani katika shule zetu,” alisema Mumba.

0 comments