Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Viongozi Arusha wamsusia Lema

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

KATIKA hali inayoonyesha kuwa mgawanyiko wa kisiasa bado unaitafuna wilaya ya Arusha jana viongozi wa serikali ngazi ya wilaya na mkoa wa Arusha walisusia hafla fupi iliyoandaliwa na mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Hafla hiyo ilikuwa inahusu ofisi ya mbunge huyo kukabidhisha msaada wa ada za shule na bima za afya kwa watoto 400 kutoka kata za Manispaa ya Arusha ambao wazazi na walezi wao hawajiwezi kimaisha.
Akizungumza kwa masikitiko, Lema alisema tendo hilo ni la maendeleo kwa jamii za Kitanzania na kwamba viongozi wote wa serikali mkoani hapa walipata mwaliko wa kushuhudia, lakini hakuna aliyefika zaidi ya mkuu wa kituo cha polisi cha Arusha.
Alisema kwa mtazamo huo dhana ya kuwakwamua Watanzania itakuwa ngumu kufanikiwa, kwani kama viongozi wa serikali wanaweza kususia jambo muhimu kama hilo, hakuna jambo linaloweza kusonga mbele.
Awali, Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo la Arusha, Elifuraha Mtowe, alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kufanya tathmini na kugundua kuwa watoto wengi wanakosa elimu kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha.
Tags:

0 comments

Post a Comment