MBUNGE mstaafu wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya, amesema baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamechoka, hawana upeo na mbinu za kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii.
Wakati Mzindakaya akitoa kauli hiyo jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, amesema wajumbe wa vikao vikubwa vya chama hicho ni wazee waliokaa madarakani kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Dk. Bana ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Taasisi ya Utafiti ya Mambo ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Redet), wajumbe hao hawana jambo jipya na wala hawawezi kuibua hoja zinazoweza kukisaidia chama hicho.
“Ndani ya vyombo hivi (vikao vya juu ) huoni CCM ya kuibua hoja mpya, wala kujibu hoja za wapinzani kwa ustadi na hii inatokana na udhaifu uliopo," alisema Dk Bana.
Alisema wazee waliojazana kwenye vikao hivyo, hawawezi kuhimili upepo wa kisiasa uliopo sasa; kwani wengi wamekaa madarakani kwa muda mrefu hali inayowafanya wasifikiri mambo mapya kwa haraka.
Dk. Mzindakaya katika hoja hiyo, alisema maendeleo ya nchi hayaletwi na Rais, bali ni viongozi walioaminiwa katika ngazi mbalimbali wakishirikiana na wananchi katika kutatua matatizo yao.
Akitoa mfano wa mkoa wa Rukwa, Dk. Mzindakaya ambaye alizungumza na waandishi wa habari jana, alisema umefanikiwa kuwa na mazao ya ziada na kuchangia katika Hifadhi ya Chakula ya Taifa zaidi ya tani milioni moja “Sisi viongozi na wananchi wa Rukwa hatukusubiri Rais aje atufanyie hayo, tulijipanga vizuri tukachagua njia ya kufuata.
Leo hii maendeleo yanaonekana kuwa ni tatizo la baadhi ya watu wanaodhani nchi ni Dar es Salaam. Tembeleeni mikoani mwone jinsi watu wanavyochapa kazi,” alisema.
Akifafanua aina ya uchovu wa baadhi ya viongozi, Dk. Mzindakaya alisema haipendezi kuona Watanzania wanaishi katika nyumba za tembe katika karne ya 21 huku kiongozi wa eneo hilo akiona ni sawa tu.
“Leo hii Rukwa hakuna tena tembe hata moja. Tuliamua tukaweza. Tabu ya viongozi wachovu ni kwamba hawataki kung’atuka hata pale wanapogundua kuwa hawana wazo jipya kusaidia maendeleo ya nchi,” alisema.
Akiwaasa wabunge wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano, mwanasiasa huyo mkongwe alisema wana wajibu wa kukemea rushwa kwa nguvu zote. Alisema Bunge linapoitwa Bunge Tukufu ni lazima waliomo ndani waukaribie huo utukufu na kujiuliza nini wamelifanyia Taifa.
“Haiwezekani kuitwa mheshimiwa wakati unafanya mambo ya hovyo hovyo. Uheshimiwa umepatikana kwa kura za wananchi. Unapokuwa bungeni, tetea masilahi ya nchi na watu waliokuchagua si vinginevyo,” alisema Mzindakaya.
Alisema mapambano dhidi ya rushwa hayana mbadala na anayekemea rushwa afanye hivyo kwa dhati ya moyo wake bila woga au kumwonea mtu.
“Utendaji wa kiongozi katika ngazi yoyote utakuwa kipimo halisi iwapo anafaa kuchaguliwa tena katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 au la. Siri ya kukubalika sasa hata baadaye ni kutumikia wananchi na kuwatendea haki. CCM ni chama changu daima na kukosoa baadhi ya mambo haina maana nakichukia, hapana,” alisema.
Kuhusu rushwa, Profesa Samuel Mushi pia wa UDSM alisema CCM isipopiga vita rushwa, itatoa taswira mbaya kwa wananchi na kuonya, “hawa wabunge wanaopinga ufisadi, wasionekane ni maadui au wahujumu chama kama tulivyoona kwenye Bunge lililopita, matendo kama haya yanaonesha kuwa CCM ni rafiki wa mafisadi.”
Kuhusu nini kifanyike, Dk. Bana ambaye alisema haoni mtu ndani ya CCM anayeweza kumrithi Rais Kikwete, alishauri Rais huyo aongoze Serikali kwa miaka mitatu na atumie kipindi kilichobaki kuimarisha chama na mambo mengi ya Serikali amwachie Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Dk. Mzindakaya yeye alisema wakati umefika kwa baadhi ya viongozi kung’atuka na kuwaachia wenye mawazo mapya kuongoza. “Mimi nimestaafu utumishi wa umma lakini si siasa mpaka umri wangu wote.”
Alimpongeza Rais Kikwete kwa kuwa kiongozi mwenye upendo kwa Taifa, mwenye upeo na nia ya kufikia hatua kubwa kimaendeleo.
“Ninyi nyote mnakumbuka Rais alisema atakapomaliza muda wake, atapenda kuacha kumbukumbu. Tayari utekelezaji wa azma hiyo umeanza katika ujenzi wa barabara, elimu, huduma za afya na uzalishaji wa kisasa shambani kupitia Kilimo Kwanza,” alisema.
Alipoulizwa endapo wasaidizi wa JK wana upeo kama alionao kiongozi huyo wa nchi, Dk. Mzindakaya alisema, “nina hakika yeyote aliyeteuliwa na Rais katika ngazi yoyote hatafanya uzembe.
Tuwape muda wateule hao, ninaamini watatenda kazi zao ipasavyo.” Lakini Profesa Mushi alisema kama kweli kuna dhamira ya kukifumua chama hicho (CCM), watu wenye tuhuma za rushwa wanapaswa kuvuliwa nyadhifa zote za uongozi ili wabaki kuwa wanachama wa kawaida.

0 comments