Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Bunge sasa kubadilisha kanuni za uundwaji wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KAMATI ya Kanuni ya Bunge jana iliridhia mabadiliko ya kanuni kwa kufanya kambi rasmi ya upinzani kubeba vyama vyote na sio Chadema pekee.

Hatua hiyo ya Kamati ya Kanuni tayari imelalamikiwa na Chadema kwamba ina lengo la kukidhofisha chama hicho.

Katika kikao leo Bunge leo linatarajia kufanya marekebisho ya baadhi ya kanuni ikiwamo ya tafsiri mpya ya kambi rasmi ya upinzani.

 Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Kamati ya Kanuni ambayo pia Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe alihudhuria baada ya mabadiliko hayo, kamati zote za kudumu za usimamizi wa fedha zitagombewa na vyama vyote vya upinzani.

Lakini, jana Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge na Halmashauri ya Chadema, John Mrema wamepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda inayoeleza nia ya Bunge kuondoa neno kambi rasmi ya upinzani bungeni ili kufanyia marekebisho.

"Tumepata taarifa kuwa Spika wa Bunge kwa kutumia nyongeza ya (8) ya kanuni chini ya kanuni ya 115 “kamati za kudumu zisizo za sekta” kifungu cha 3 (1) kinachompa mamlaka ya kuunda Kamati ya kubadili Kanuni za Bunge aliunda kamati hiyo yenye lengo la kufanya marekebisho ya Kanuni za Bunge,”alisema Mrema.

Mrema alisema Chadema kimegundua kuwa miongoni mwa sababu za kuundwa kwa kamati hiyo ni kutaka kufanyia mabadiliko kipengele hicho ambacho kitapunguza nguvu ya upinzani bungeni na zaidi nguvu ya Chadema ambacho ndicho chama chenye sifa za kusimamia na kuhoji Serikali.

Alisema kwa mujibu wa utamaduni wa mabunge ya Jumuiya za Madola, chama kikuu cha upinzani ndicho chama mbadala wa chama tawala na kina sifa za kusimamia na kuhoji Serikali juu ya mambo mbalimbali hasa kwenye kamati tatu za Bunge zinaofahamika kama Kamati za Kudumu za Bunge.

Kwa mujibu wa kanuni za sasa, wabunge walio nje ya kambi rasmi ya upinzani bungeni hawaruhusiwa kuingia na kuongoza kamati hizo tatu za Bunge ambazo ni za mashirika ya umma, serikali na mitaa na ile ya hesabu za serikali.

“Mara baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika wa mwaka 2010, Chadema tulipata wabunge wengi ambao walikiwezesha chama kuwa na haki ya kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kifungu cha 14 kifungu kidogo cha 3,”alisema Mrema.

Mrema alifafanua kuwa mabadiliko hayo ya kanuni yanafuatia barua ilioyoandikwa na vyama vingine vya upinzani vikiongozwa na CUF kwenda kwa Spika na kutaka neno kambi rasmi ya upinzani bungeni lifutwe.

Alisema lengo la vyama hivyo ambavyo kwa sasa havikuwa na sifa ya kuunda kambi ya upinzani bungeni na havikushirikishwa kwenye kambi iliyoundwa na Chadema ni kutaka kuwa na haki ya kuunda umoja wao unaojulikana kama minority camp.


Wakati chama hicho kikitoa maelezo yake hayo habari za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya vikao vya vyama vya siasa na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge zilisema kuwa moja ya kanuni zitakazorekebishwa ni ile inayotambua uwepo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Kanuni hiyo inatoa nafasi kwa chama cha upinzani kinachofikisha asilimia 12.6 ya wabunge kuwa kambi rasmi ya upinzani ambapo kwa sasa ni Chadema yenye wabunge takribani 70.

Hali hiyo iliviacha kando vyama vingine vya CUF, NCCR, TLP, UDP vyenye wabunge wachache vikilalamika kutoshirikishwa katika kambi hiyo hivyo kuzua mvutano vikiitana kuwa na kambi yake ndogo ya upinzani.

Iwapo mabadiliko hayo yatatokea vyama vya upinzani vitakuwa vimefungishwa 'ndoa' ya lazima baada ya kulumbana kuhusu nafasi ya kambi yao.
Tags:

0 comments

Post a Comment