Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Muumini wa dini ya Kikristo awataka Maaskofu wake kuvua majoho

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Muumini wa dini ya Kikristo Mary Chatanda ambaye pia ni Katibu wa CCM mkoa wa Arusha amewataka Maaskofu wake kuvua majoho  ya kazi yao na kutangaza kuingia katika siasa. 

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wa Jiji la Arusha na kuwataka maaskofu hao kuacha kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha. 

Chatanda alisema, kitendo cha maaskofu kusema hawamtambui Meya wa CCM Arusha, Gaudence Lyimo kimewashtua na hakiwezi kuachwa hivi hivi. 
Alisema viongozi wa dini wanapoingilia masuala ya siasa ni ukiukwaji wa majukumu yao hivyo bora wavue majoho yao na kuingia kwenye ulingo wa siasa kama alivyofanya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa. 

Chatanda ambaye ndiye anatajwa kuwa chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha, hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa kama Mbunge mkoani Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa wenyewe. 

Chatanda ambaye alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani na kuwataka waumini kuwa wacha Mungu na si kushabikia siasa. 

"Sisi kama viongozi wa CCM wa Mkoa wa Arusha tumesikitishwa na kauli za maaskofu hao na tulitegemea kabla ya kutoa tamko lao wangetuita sote na tukatoa maelezo yetu na hapo ukweli wangeupata lakini kusema uchaguzi haukuwa halali si sawa." 

Hata hivyo, alisema yeye kama Mbunge, alipangiwa na chama chake kuwa Arusha na hivyo, ataendelea kuwa diwani wa CCM Arusha hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na chama chake. 

Akizungumzia makundi ndani ya CCM ambayo pia yanampinga hasa kutokana na kumtuhumu kusababisha CCM kushindwa Jimbo la Arusha, alisema wanaCCM hao hawajui wanalosema hivyo wanapaswa kusamehewa. 

Juzi Maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba hawatampa ushirikiano meya huyo. 


Sent from my iPhone
Tags:

0 comments

Post a Comment