Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Tamisemi waunda Tume kunasa waliochota fedha za Serikali

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter WAJANJA wachache wakiwamo baadhi ya watendaji waandamizi wa halmashauri za wilaya katika Mkoa wa Morogoro, wamefuja mamilioni ya fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Miradi ambayo fedha hizo zimeliwa na wajanja wachache ni pamoja na ya ujenzi wa zahanati, machinjio, masoko na nyumba za watumishi.

Kutokana na ubadhirifu huo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeunda timu ya kufuatilia kwa kina ufujaji huo itakayoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wake , Eliamikimu Maswi.

Lengo la timu hiyo ni kubaini wahusika na ubadhirifu na wizi wa fedha za Serikali kupitia miradi hiyo.

Uamuzi huo umetolewa juzi na Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri wakati akitoa majumuisho ya ziara aliyoifanya mkoani Morogoro baada ya kuzitembelea halmashauri zote sita za mkoa huo.

Ziara hiyo maalumu ililenga kufuatilia na kukagua baadhi ya miradi kwa ajili ya kutafuta thamani halisi ya fedha zinazotolewa na Serikali Kuu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii.

“ Timu hii itafanya uchunguzi wa kina katika miradi yote yenye dosari kwenye baadhi ya halmashauri kwa ‘kupekenyua’ mikataba na hati za manunuzi ya vifaa zilizoidhinishwa na taarifa yake ndiyo itakayotumika kuwachukulia hatua watakaobainika ,“ alisema Naibu
Waziri huyo.

Timu hiyo itaanzia Kilosa, kwenye miradi miwili ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Palakuyo inayoonesha ilitumia Sh milioni 100 bila kukamilika, machinjio yaliyojengwa Kata ya Kimamba A kwa gharama ya Sh milioni 30 na kubomoka kabla hata ya kuanza kutumika kuchinja wanyama.

Waliofariki ajali ya Sumry watambuliwa Na John Nditi, Morogoro WATU saba kati ya nane
waliofariki katika ajali ya basi la Sumry iliyotokea kwenye barabara kuu ya Morogoro-Iringa juzi, katika Kijiji cha Masimba, wametambuliwa na ndugu zao na miili yao kuchukuliwa.

Ajali hiyo ilitokea eneo hilo katika Tarafa ya Mikumi, wilayani Kilosa saa 9 alasiri baada ya kugongana na lori aina ya Fuso mali ya Kampuni ya kutengeneza pipi ya Ivory lilipokuwa likitokea mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam juzi.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Morogoro, Ibrahim Mwamakula alithibitisha kutambuliwa kwa maiti hao na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya maziko katika maeneo mbalimbali.

Alisema ajali hiyo ilihusisha basi hilo aina ya Nissan lenye namba T333 BCX lililokuwa likitokea mkoani Dar es Salaam kwenda Iringa na lori hilo aina ya Fuso lenye namba T 317 ASR.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, maiti waliotambuliwa ni Abubakar Laiser ( 25) ambaye ni Ofisa Masoko na mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, Mariam Jaha ( 25) Mhasibu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Iringa, Mboko Anyasime (31) Ofisa wa Mifugo na mkazi wa Iringa.

Wengine ni Saddiq Lyimo ambaye ni mtumishi wa Bohari ya Taifa ya Madawa (MSD) mkazi wa Dar es Salaam, Happy Alfred Mwakonjombe (15) Mkazi wa Iringa na Vicent Mrema (35) mfanyabiashara na Mkazi wa Kimara Dar es Salaam.

Wengine ni Doris Lwungo ( 24) mkazi wa Ipogoro mkoani Iringa na Martin Cassian ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Idiogoya ya mjini Iringa.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo mwili wa Martin Cassian bado umehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kutokana kukosa ndugu wa kuutambua na kuthibitisha.

Majeruhi wote 21 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya St Kizito mjini Mikimu waliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na kupata nafuu.
Tags:

0 comments

Post a Comment