Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Katibu wa balozi wa Vatican afa maji Dar

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
UBALOZI wa Vitican nchini umepata pigo baada ya Katibu wa Balozi Degny Alain Maxime (35) na mhasibu wake raia wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la Padre John (59), kufa maji.

Maxime ambaye ni raia wa Ivory Coast na John, raia wa Ujerumani anayeishi Kurasini katika majengo ya Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), walifariki baada ya kuzama kwenye Bahari ya Hindi. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa raia hao wa kigeni, walizama kwenye bahari hiyo wakati walipokuwa wakiogelea katika ufukwe wa Hoteli ya Kasa.  Alisema raia hao walifika katika hoteli hiyo juzi saa 5.00  asubuhi wakiwa wateja wa nje ambao walikuwa wakitumia gari aina ya Land Rover 110 S’wagon.

Kwa mujibu wa kamanda Shilogile, watu hao baada ya kufika hotelini hapo walikwenda kuogelea katika eneo hilo na hatimaye kuzama na kunywa maji mengi ambayo yaliwasababishia kifo.

Alisema maiti zao ziliopolewa jioni ya saa 10.30 na maiti zao zimehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea.  

Katika tukio jingine, Mkazi wa Magomeni, Saada Imani (25) alifariki dunia kwa kugongwa na gari juzi usiku wakati alipokuwa akivuka barabara ya Nyerere eneo la Tazara jijini Dar es salaam.

  Kamanda Shilogile alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 6.25 usiku katika barabara hiyo ambapo dereva na gari lisilofahamika aliyekuwa akitokea Tazara kuelekea Vingunguti alimgonga mtembea kwa miguu huyo na kufariki dunia.

 Shilogile aliongeza maiti ya marehemu huyo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Amana na upelelezi wa kulisaka gari na dereva aliyesababisha kifo cha dada huyo unaendelea. 
Tags:

0 comments

Post a Comment