Habari kwa hisani ya Mwananchi WAZIRI Mkuu wa zamani, John Malecela, amesema kuwa CCM imewakosea adabu maaskofu hivyo inapaswa kukutana nao na kuwaomba radhi.Akizungumza na Mwananchi jana, Malecela alisema kitendo cha kuwashambulia maaskofu hao kilichofanywa na CCM mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kuwataka wavue majoho na kuingia kwenye siasa, ni utovu wa nidhamu. Kauli ya Malecela ambaye pia ni kada wa CCM, imekuja siku mbili baada ya chama hicho mkoani Arusha kuwataka maaskofu mkoani humo, kuvua majoho na kutangaza kuingia kwenye siasa, badala ya kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha. Januari 7 mwaka huu, maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha, walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba "hawatampa ushirikiano". Walitoa tamko hilo wakati wakilaani hatua ya polisi mkoani Arusha kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 20. Akisoma tamko la umoja wa viongozi wa dini ya Kikristo mkoani Arusha, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu alisema Jeshi la Polisi ndilo lilikuwa chanzo cha vurugu hizo. "Sisi kama viongozi wa dini hatuwezi kushirikiana na mtu ambaye hakushinda kihalali, kuna mtu alipiga kura si diwani wa Arusha, Chadema hawakushirikishwa na pia taratibu na kanuni za uchaguzi huo zilikiukwa," alisema askofu huyo. Lakini, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa kitendo cha maaskofu hao kusema hawamtambui Meya wa CCM, Gaudence Lyimo, kimewashtua. "Tunawaheshimu sana viongozi wa dini...Ila wanapoingilia masuala ya siasa ni bora wavue majoho tukutane viwanja vya siasa kama alivyofanya mwenzao Dk Slaa," alisema Chatanda. Katibu huyo ambaye ndiye chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa. Chatanda ambaye katika mkutano huo alikuwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Onesmo Ole Nangole, alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani za kwenda mbinguni na sio siasa. "Waje kwenye siasa wagombee udiwani...ili wachague meya. Tulitegemea kabla ya tamko lao wangetuita sote na tukae na tutoe maelezo yetu na hapo ukweli wangeupta, lakini kusema uchaguzi haikuwa halali sio kweli," alilalamika Chatanda. Wakati katibu huyo wa mkoa wa CCM akieleza hayo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alienda mbali zaidi na kuwataka maaskofu hao waende mahakamani au wawashauri Chadema kufanya hivyo kwa lengo la kupinga matokeo ya umeya. Makamba alisisitiza kuwa msimamo wa CCM ni kwamba chama hicho ndicho kilichoshinda katika uchaguzi huo wa umeya Arusha. Alisema hakuna njia ya kubadili matokeo hayo zaidi ya kufungua kesi mahakamani. Lakini jana Malecela alisema CCM inatakiwa kutumia busara kushughulikia mgogoro wa umeya mkoani Arusha badala ya jazba na utovu wa nidhamu. Alisema kauli ya katibu huyo wa CCM dhidi ya maaskofu inakera na ili kuweka mambo sawa, ni bora chama hicho tawala kiwaombe radhi viongozi hao wa dini. "Ni wazi kwamba alichokisema Chatanda hakiwezi kuwa kauli ya chama. Hayo ni maneno yake na ni utovu wa nidhamu. Nasikitika sana kauli ni ya kwake na si ya chama hivyo aombe radhi," alisema Malecela ambaye alibainisha kuwa chama cha siasa hakina uwezo wa kuwataka maaskofu wavue majoho. Kwa mujibu wa Malecela, viongozi wa dini wako tangu enzi za kale na wamekuwa wakiikosoa Serikali tangu wakati huo na haiajawahi kutokea kiongozi wa chama akawarukia kwa maneno makali kiasi hicho. Malecela alisema hiyo sio kauli ya CCM, lakini kwa kuwa imetolewa na mwanachama wake, chama hakina budi kukutana na viongozi hao wa dini na kuwaomba radhi. Kauli iliyotolewa ni ya kutokuwa na adabu kwa watu kama maaskofu," alisema Malecela. |
You Are Here: Home - - Malecela: CCM imekosa adabu kwa maaskofu
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Comments
nadhani huu bwana hajui anachochangia. ni kilaza mkubwa na anafuata mkumbo hajaona busara za mzee malechela.
Wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa nchi inapelekwa pabaya. Udini una shamiri. Mhariri wa gazeti hili usije ukalalamika ukaja kupelekwa The Hague kwa uchochezi.
Hebu fikiria, Pemba waliuwawa na polisi watu zaidi ya 21 katika mazingira kama haya. Wengine wakawabakwa na wengine kuwa wakimbizi. Hatujasikia Maaskofu kulaani mauaji hayo. Kwa nini sasa? Je, muislamu a[NENO BAYA]sea kuwa Maaskofu hawakulaani vitendo hivyo kwa kuwa Rais wakati huo alikuwa Mkristo?
Nao wanaharakati wanaojiita watetezi wa haki za binadamu hawajafanya lolote kwa vile wwengi wa wanaharakati hawa ni wakirsto. Lakini wanaharakati hawa waliandamana kupinga hukumu aliepewa muislamu wa Nigeria aliehalifu amri ya imani ya dini yake mwenyewe.
Mnatupeleka mbali na kubaya. Vueni majoho muingie siasa msichochee udini. Vurugu za dini ni mbaya zaidi na nchi itakuwa haitwaliki hii.
Chonde chonde mti na macho
"Wakristo wanaipeleka hii nchi pabaya"
Huu uliofanya ndio Udini ndugu Nduli...! Comment kama za kwako ni za kuogopwa kuliko matamshi ya maaskofu..! Na Kama unataka Serikali ifanye inavyotaka..na viongozi wa dini wakae kimya..Unataka nini? Mtu yeyote anayekeme uovu...Huyo ni mtu sahihi...! Na kwa taarifa yako..Viongozi wa Kiislamu wametoa tamko kama hilo pia..Unasemaje hapo? Unapotea sana ndugu...Na sidhani kama unaitakia mema nchi yetu.
Viongozi wa dini kama vililvyo NGO's nyingine ni kama washauri na wakemeaji pale mambo yanapokwenda kinyume na utaratibu, mfn hilo la uchaguzi wa meya wa Arusha.
Sijui Serikali inasubiri nini mpk muda huu! Chatanda kutoa maneno ya kashfa kwa maaskofu. Badala CCM kumkemea wametia mafuta ugomvi huo kupitia Makamba kama msemaji mkuu wa chama hicho. Kwa hiyo CCM ngazi ya mkoa na taifa wamemunga mkono mawazo ya Chatanda.
Hivo inadhiirisha kiasi gani serikali aielewi wajibu wake kwenye maswala ya malumbano ya kisiasa, bali wanachojua ni kutumia police kuzuia maandamano ya wapinzani.
Hili swala litaleta mengi, hivo kuzuia inabidi Chatanda na Makamba kuanchia nafasi zao ukatibu na kuomba radhi kwa kauli zao.
Na pia anayengangania umeyawa Arusha kuachia nafasi hiyo ili kuwezesha uchaguzi kufanyika mapema iwezekanavyo.
Serikali na CCM wasipoangalia wataipeleka nchi hii pabaya, kwani wanaendeleza chuki baina ya wananchi. hivo inabidi kukemea mchezo huu mchafu
Tusisahau kwamba njia ya kutatua wenyewe ni kuunga wapinzani 2015 na Katiba Mpya
Quoting Nduli-la-Mizimwi:
hivi huyo mama anamatatizo gani, damu inamwagika kwa ajili yake na bado haoni na anazidi kuropoka mi nahisi imeanza kula kwake coz hata yeye mwenyewe hajielewi anaongea nini.
poleni sana wananchi wa arusha kwa yaliyo wapata namini malipo yenu yapo yanakuja. huo ndo mwisho wa wanyonyaji na mwanzo wamatumaini
CCM mlitawala miaka karibia hamsini sasa hamuoni watu wamechoka na siasa zenu za ubinabsi na uonevu. Naona sasa watanzania tumwachie Mungu ndiye muamuzi wa yote.
Kwanza inavyoonekana yeye ndiye chanzo cha vurugu zote.
hafai na inatakiwa awajivishwe.