Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kituo cha sheria chafichua siri Dowans

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimefichua siri ya mgogoro kati ya Shirika la Ugavi wa Umeme la Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya  Kufua Umeme ya Dowans kuhusu malipo ya shilingi  bilioni 94 zinazotaka kulipwa kwa kampuni hiyo.

Afisa Mwandamizi wa LHRC, Harold Sungusia amesema kituo hicho kimelazimika kufungua shauri namba 4 la mwaka 2010 kwenye Kitengo cha Biashara cha Mahakama Kuu ya Tanzania ili kuizuia TANESCO kuilipa Dowans mabilioni hayo ya fedha chini ya hukumu yenye utata iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC).

Kituo hicho kilifungua shauri hilo dhidi ya Dowans Tanzania Limited (DTL), kama mdaiwa wa kwanza, Dowans Holdings (Costa Rica) kutoka Afrika Kusini, kama mdaiwa wa pili, na pia TANESCO, kama mdaiwa wa tatu, kufuatia hukumu ya ICC ya kulazimisha shirika hilo la umma kulipa fedha hizo kwa kuwakamua Watanzania.

“Tunapinga hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo (ICC) kwa kuwa ni batili kutokana na ukweli kwamba maamuzi yake hayakuwa sahihi,” alisema Afisa Mwandamizi wa kituo hicho, Harold Sungusia na kuongeza kuwa kituo hicho kimebaini uonevu katika shauri hilo dhidi ya wadaiwa wote watatu.

Katika kuthibitisha kuwa usuluhishi huo ulikuwa wa hovyo, kimetaja jopo la majaji watatu walioketi kuwa ni Sir Jonathan Parker, Swithin Munyantwali na aliyekuwa mwenyekiti wa jopo hilo, Sir Gerald Aksen.

Kimesisitiza kuwa jopo la majaji hao walifikia uamuzi wa kuipendelea kampuni hiyo ya kigeni wakati iliingia mkataba wa kitapeli na shirika hilo la umma.

Tayari Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (pichani)  ameshatoa tamko kuwa  serikali itailipa Dowans shilingi Bilioni 94.
Tags:

0 comments

Post a Comment