Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Changa la Macho Lingine: Gari la kubeba fedha lagonga Treni

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter


Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya gari aina ya Hiace lenye namba za usajili T 151 BGJ kugongwa na kichwa cha treni kilichokuwa kikivuka  Bararaba ya Korogwe jirani na ofisi za Tanesco Manispaa ya Morogoro leo.
 GARI la CRDB Bank lililotumika kuleta fedha mkoani Morogoro kutoka Dar es Salaam, mchana wa leo limegongwa na treni eneo la Tanesco katika Manispaa ya Morogoro wakati linaelekea Dar es Salaam kuchukua fedha.

Gari hilo aina ya Hiace lenye namba za usajili T 151 BGJ liligongwa na kichwa cha treni kilichokuwa kikivuka  Bararaba ya Korogwe jirani na ofisi za Tanesco mjini hapa na kuburuzwa umbali wa mita 50 ambapo kwa mujibu wa habari zilizopatikana eneo la tukio zilidai kwamba katika ajali hiyo hakuna mtu aliyekufa lakini dereva wake aliumia  vibaya.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Morogoro, lbrahimu Mwamakula, alifika eneo la tukio na kuwaomba vijana waliokuwepo eneo hilo kuliondoa gari hilo kwenye reli.

Vijana hao walitii agizo hilo wakitegemea kungekuwa na ujira baada ya kumaliza kazi hiyo.

Baada ya kumaliza kazi hiyo, vijana hao walimsaka ofisa huyo wa polisi ambaye baada ya kutoa agizo hilo alitoweka eneo la tukio na kwamba vijana hao baada ya kumkosa walimzonga trafiki aliyekuwa akipima ajali hiyo wakimtaka awalipe ujira wao.

Hata hivyo, afande huyo hakuonesha hali ya kujali mkwara wa vijana hao.   Hadi mtandao huu unaondoka eneo hilo, bado muafaka wa jambo hili ulikuwa  haujapatikana.

Aidha baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo walisikika wakisema kwamba gari hilo la fedha kama lingekuwa linatoka Dar es Salaam na lundo la pesa na kupatwa na ajali hiyo, hali ingekuwa tofauti.
Zifuatazo ni picha za tukio hilo:
 


PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE, /GPL,  MOROGORO
Tags:

0 comments

Post a Comment