Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Malecela: CCM imekosa adabu kwa maaskofu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Habari kwa hisani ya Mwananchi
WAZIRI Mkuu wa zamani, John Malecela, amesema kuwa CCM imewakosea adabu maaskofu hivyo inapaswa kukutana nao na kuwaomba radhi.Akizungumza na Mwananchi jana, Malecela alisema kitendo cha kuwashambulia maaskofu hao kilichofanywa na CCM mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kuwataka wavue majoho na kuingia kwenye siasa, ni utovu wa nidhamu.

Kauli ya Malecela ambaye pia ni kada wa CCM, imekuja siku mbili baada ya chama hicho mkoani Arusha kuwataka maaskofu mkoani humo, kuvua majoho na kutangaza kuingia kwenye siasa, badala ya kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

Januari 7 mwaka huu, maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha, walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba "hawatampa ushirikiano".

Walitoa tamko hilo wakati wakilaani hatua ya polisi mkoani Arusha kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

Akisoma tamko la umoja wa viongozi wa dini ya Kikristo mkoani Arusha, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu alisema Jeshi la Polisi ndilo lilikuwa chanzo cha vurugu hizo.

"Sisi kama viongozi wa dini hatuwezi kushirikiana na mtu ambaye hakushinda kihalali, kuna mtu alipiga kura si diwani wa Arusha, Chadema hawakushirikishwa na pia taratibu na kanuni za uchaguzi huo zilikiukwa," alisema askofu huyo. 

Lakini, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa kitendo cha maaskofu hao kusema hawamtambui Meya wa CCM, Gaudence Lyimo, kimewashtua.

"Tunawaheshimu sana viongozi wa dini...Ila wanapoingilia masuala ya siasa ni bora wavue majoho tukutane viwanja vya siasa kama alivyofanya mwenzao Dk Slaa," alisema Chatanda.

Katibu huyo ambaye ndiye chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa.

Chatanda ambaye katika mkutano huo alikuwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa,  Onesmo Ole Nangole, alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani za kwenda mbinguni na sio siasa.

"Waje kwenye siasa wagombee udiwani...ili wachague meya. Tulitegemea kabla ya tamko lao wangetuita sote na tukae na tutoe maelezo yetu na hapo ukweli wangeupta, lakini kusema uchaguzi haikuwa halali sio kweli," alilalamika Chatanda.

Wakati katibu huyo wa mkoa wa CCM akieleza hayo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alienda mbali zaidi na kuwataka maaskofu hao waende mahakamani au wawashauri Chadema kufanya hivyo kwa lengo la kupinga matokeo ya umeya.

Makamba alisisitiza kuwa msimamo wa CCM ni kwamba chama hicho ndicho kilichoshinda katika uchaguzi huo wa umeya Arusha.

Alisema hakuna njia ya kubadili matokeo hayo zaidi ya kufungua kesi mahakamani.

Lakini jana Malecela alisema CCM inatakiwa kutumia busara kushughulikia mgogoro wa umeya mkoani Arusha badala ya jazba na utovu wa nidhamu.

Alisema kauli ya katibu huyo wa CCM dhidi ya maaskofu inakera na ili kuweka mambo sawa, ni bora chama hicho tawala kiwaombe radhi viongozi hao wa dini.

"Ni wazi kwamba alichokisema Chatanda hakiwezi kuwa kauli ya chama. Hayo ni maneno yake na ni utovu wa nidhamu. Nasikitika sana kauli ni ya kwake na si ya chama hivyo aombe radhi," alisema Malecela ambaye alibainisha kuwa chama cha siasa hakina uwezo wa kuwataka maaskofu wavue majoho.

Kwa mujibu wa Malecela, viongozi wa dini wako tangu enzi za kale na wamekuwa wakiikosoa Serikali tangu wakati huo na haiajawahi kutokea kiongozi wa chama akawarukia kwa maneno makali kiasi hicho.

Malecela alisema hiyo sio kauli ya CCM, lakini kwa kuwa imetolewa na mwanachama wake, chama hakina budi kukutana na viongozi hao wa dini na kuwaomba radhi. 

Kauli iliyotolewa ni ya kutokuwa na adabu kwa watu kama maaskofu," alisema Malecela.


Comments 






0#26 Johnn Kisale 2011-01-10 12:15
Quoting Nduli-la-Mizimwi:
Wakristo wanaipeleka hii nchi pabaya. Hii vita ya kichinichini na kufichaficha haitakuwa na mema kwenu pamoja na wote wengineo. Leo wapo wengi wasio wakristo wanaounga mkono harakati za Chadema dhidi ya serikali lakini kila kukicha ukweli unazidi kuthibitika kwamba nia na malengo ya upinzani unaoendelea ni udini wala sio siasa. Shauri yenu watanganyika. Msiendeshwe na Maaskofu wenye malengo ya kurudisha ubwana walio u-enjoy enzi ya Mchonga meno. Haiwezekani mkarudi enzi za kale kwenye ulingo wa sasa, ngoma inayochezwa ni tofauti na ya uwazi. Kweli vueni hayo majoho muingie kwenye uwanja wa siasa. Porojo zenu zimejulikana.

nadhani huu bwana hajui anachochangia. ni kilaza mkubwa na anafuata mkumbo hajaona busara za mzee malechela.
-1#25 Mkombe Sillima 2011-01-10 12:13
Mimi nashangaa sana na kelele za Maaskofu na Malecela. Hawa wote ni wanafiki. Sumbawanga wamesimamishwa waumini kwa makosa yanayodaiwa ni ya imani. Askofu walikuwa na haki ya kuingilia uhuru wa kuchagua wa waumini wao. Tena kipi kibaya na wao wanapoteleza wasielezwe. Si kweli kama maaskofu na mashehe hawajapata kuambiwa wavue majoho kama wanataka kujiingiza mambo ya siasa chini ya kichaka cha kanisa. Malecela anamajeraha aliyoyapata ya kukosa ubunge na anaelekeza hasira zake kwa chama kilichomkataa cha CCM.

Wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa nchi inapelekwa pabaya. Udini una shamiri. Mhariri wa gazeti hili usije ukalalamika ukaja kupelekwa The Hague kwa uchochezi.

Hebu fikiria, Pemba waliuwawa na polisi watu zaidi ya 21 katika mazingira kama haya. Wengine wakawabakwa na wengine kuwa wakimbizi. Hatujasikia Maaskofu kulaani mauaji hayo. Kwa nini sasa? Je, muislamu a[NENO BAYA]sea kuwa Maaskofu hawakulaani vitendo hivyo kwa kuwa Rais wakati huo alikuwa Mkristo?

Nao wanaharakati wanaojiita watetezi wa haki za binadamu hawajafanya lolote kwa vile wwengi wa wanaharakati hawa ni wakirsto. Lakini wanaharakati hawa waliandamana kupinga hukumu aliepewa muislamu wa Nigeria aliehalifu amri ya imani ya dini yake mwenyewe.
Mnatupeleka mbali na kubaya. Vueni majoho muingie siasa msichochee udini. Vurugu za dini ni mbaya zaidi na nchi itakuwa haitwaliki hii.

Chonde chonde mti na macho
0#24 Godfrey 2011-01-10 12:11
Nduli-la-Mizimwi 2011-01-10 10:27
"Wakristo wanaipeleka hii nchi pabaya"

Huu uliofanya ndio Udini ndugu Nduli...! Comment kama za kwako ni za kuogopwa kuliko matamshi ya maaskofu..! Na Kama unataka Serikali ifanye inavyotaka..na viongozi wa dini wakae kimya..Unataka nini? Mtu yeyote anayekeme uovu...Huyo ni mtu sahihi...! Na kwa taarifa yako..Viongozi wa Kiislamu wametoa tamko kama hilo pia..Unasemaje hapo? Unapotea sana ndugu...Na sidhani kama unaitakia mema nchi yetu.
-9#23 kihumo 2011-01-10 12:10
Hawa Maaskofu wamempika slaa na walisubiri kula ndiyo maana wana lalamika maana walijua mtoto wao (Slaa) atakuwa raisi kwa hiyo tafakarini. Wamegharamia pesa nyingi sana na miaka mingi sana kumpika Slaa aje kuwa Rais wa nchi hii wao wakingali hai.
+3#22 jungu 2011-01-10 12:06
kauli ya chatanda ni ya mtu asiyesoma maandiko matakatifu kazi ya utumishi wa mungu uwe shehe au padre nikuwaongza watu kutoka maovuni na kwenda kwenye njia iliyo sahihi maaskofu walifanya kile walichotakiwa kufanya kwa kuonesha dhambi ya ccm na madhara ambayo yanatokana na dhambi iyo ambayo watu wanauawa arusha kwa kutofuata sheria ya uchaguzi wa umeya,uyo makamba uwa anasoma maaandiko ila aelewi maana yake,tumsamehe tu
-8#21 Chitakamiye 2011-01-10 12:04
Babu Usiwatetee hao maaskofu. wamezidi kuingilia mambo ya siasa hao maaskofu. Ndicho walichokuwa wanakitaka. Siasa na dini havichangamani hata siku moja. Wao walipaswa kutoa maoni lakini siyo misimamo kama hiyo. Ndo mana siku hizi kila askofu anaestaafu anagombea ubunge. Wamekumbwa na pepo wa siasa na tifu la siasa ndo hilo. Hakuna utovu wa nidhamu hapo.
+5#20 Katiba TANGANYIKA 2011-01-10 11:58
Alichosema Mzee Malecela ni kweli.

Viongozi wa dini kama vililvyo NGO's nyingine ni kama washauri na wakemeaji pale mambo yanapokwenda kinyume na utaratibu, mfn hilo la uchaguzi wa meya wa Arusha.

Sijui Serikali inasubiri nini mpk muda huu! Chatanda kutoa maneno ya kashfa kwa maaskofu. Badala CCM kumkemea wametia mafuta ugomvi huo kupitia Makamba kama msemaji mkuu wa chama hicho. Kwa hiyo CCM ngazi ya mkoa na taifa wamemunga mkono mawazo ya Chatanda.

Hivo inadhiirisha kiasi gani serikali aielewi wajibu wake kwenye maswala ya malumbano ya kisiasa, bali wanachojua ni kutumia police kuzuia maandamano ya wapinzani.

Hili swala litaleta mengi, hivo kuzuia inabidi Chatanda na Makamba kuanchia nafasi zao ukatibu na kuomba radhi kwa kauli zao.

Na pia anayengangania umeyawa Arusha kuachia nafasi hiyo ili kuwezesha uchaguzi kufanyika mapema iwezekanavyo.

Serikali na CCM wasipoangalia wataipeleka nchi hii pabaya, kwani wanaendeleza chuki baina ya wananchi. hivo inabidi kukemea mchezo huu mchafu

Tusisahau kwamba njia ya kutatua wenyewe ni kuunga wapinzani 2015 na Katiba Mpya
+7#19 Adiue Humble 2011-01-10 11:56
Watanzania tuache kuishi kwa hisia na mazoea,mchangia ji wa kwanza anahusisha machafuko ya Arusha na udini, in fact anasema wazi ni njama ya maaskofu ambao wanataka kurudisha nchi enzi za Mwalimu ambako walikuwa wana-enjoy! Napenda kuweka historia vizuri kwa faida ya wengi: Uchaguzi wa Meya Arusha ulizua mzozo kati ya ccm na chadema siku ya kwanza kwa sababu CCM wali import mbunge wa viti maalum kutoka Tanga, Mary Chatanda jambo ambalo lilisababisha uchaguzi kuahirishwa. Siku iliyofuata madiwani wa chadema waliambiwa kuna semina ukumbi wa Olasiti wakaenda huko, kumbe huku nyuma wenzao wa ccm wakachagua meya. Chadema baada ya kusubiri bila mafanikio wakaamua kurudi ofisi za jiji zamani manispaa kuuliza kulikoni mbona wamewapeleka kule kupoteza muda? Wakiongozwa na Mbunge wao, Godbless Lema walipofika manispaa walikuta wenzao wa ccm wameshachagua meya, katika kuhoji uhuni huo, madiwani hao walimwita OCD wa Arusha kuja kumkamata Mh. Lema eti analeta fujo. Akapigwa sana mpaka akapoteza fahamu, kumbuka huyo nikiongozi wa watu anadhalilishwa mbele ya wapiga kura wake, hayo tuyaache, Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe kwa busara zake alivyoona hivyo alikwenda Arusha akatuliza hali akafanya mawasiliano na viongozi wa kitaifa akiwasihi uchaguzi urudiwe ili kuondoa hali ya vurugu, hilo halikufanyika. Mbowe akatoa muda mpaka tarehe 4 Januari kama waziri wa Tamisemi atakuwa hajatatua mgogoro huo wataandamana kulaani uvunjifu wa taratibu na kufanya mkutano wa hadhara ili kuelezea hisia zao na kutoa the way forward. Kweli hadi tarehe hiyo serikali haikufanya chochote, Chadema wakaomba ulinzi kwa IGP siku ya maandamano tarehe tano januari na baadaye kwenye mkutano wa hadhara kweli polisi wakatoa kibali, siku moja kabla ya siku ya maadamano IGP alijitokeza kwenye vyombo vya habari akitangaza kufuta kibali cha maandamano lakini akaruhusu mkutano wa hadhara. Viongozi wa chadema akiwemo Mbowe, Dr Slaa, Lema, Ndesamburo Grace Kiwelu na wengine walikuwa wamefikia katika hoteli ya Mount Meru kwa ajili ya mkutano. Siku ya tarehe tano wakaamua watembee kwa miguu kwenda uwanja wa NMC kwenye mkutano watu wakawa wanawafuata tena kwa amani hapo ndipo machafuko yalipotokea, najiuliza hisia za udini zinaingiaje hapa? Viongozi wa chadema wangeendaje kwenye mkutano, wangeruka juu angani? Ama watu wa arusha wangeendaje mkutanoni bila kutembea?
0#18 cliff 2011-01-10 11:53
hongera mzee,nahisi huyo mwanamama wa arusha na mzee makamba ni mda wao kuchakachuliwa.
+2#17 Denis kunambi 2011-01-10 11:30
Leburu ametimiza wajibu wake Kama Mchangaji awatakiaye mema kondoo wake. Serikali semeni lenu.
0#16 vuvuzelank 2011-01-10 11:30
Hili lishenzi la wapi? na hao waislamu walivyoongea walivyopinga utaaeleza nini. shwaini mkubwa wewe unaongelea udini badala ya kuleta hoja. nyie waccm ndo mnaleta udini, kwa kuwahonga waislam ili watoe tamko, mlikuwa mhangaika nini kuwahamasisha waandishi wa habari wahudhurie mkutano ambao ni tamko la waislamu Arusha. Shwaini wewe!.
Quoting Nduli-la-Mizimwi:
Wakristo wanaipeleka hii nchi pabaya. Hii vita ya kichinichini na kufichaficha haitakuwa na mema kwenu pamoja na wote wengineo. Leo wapo wengi wasio wakristo wanaounga mkono harakati za Chadema dhidi ya serikali lakini kila kukicha ukweli unazidi kuthibitika kwamba nia na malengo ya upinzani unaoendelea ni udini wala sio siasa. Shauri yenu watanganyika. Msiendeshwe na Maaskofu wenye malengo ya kurudisha ubwana walio u-enjoy enzi ya Mchonga meno. Haiwezekani mkarudi enzi za kale kwenye ulingo wa sasa, ngoma inayochezwa ni tofauti na ya uwazi. Kweli vueni hayo majoho muingie kwenye uwanja wa siasa. Porojo zenu zimejulikana.
+2#15 Ndilo Yamnyanza 2011-01-10 11:27
Hongera mzee Malecela kwa busara na hekima. Huyo binti (Mary Chatanda) anahitaji "kitchen party'maana hajui alitendalo. Kupata ubunge tu tena kwa mara ya kwanza ameshalewa na anafikiri anaweza kusema chochote kwa mtu yeyote. Hawezi kuwatukana hao wazee (maaskofu)kiasi hicho kama sio kutafuta laana. Wazee wenye hekima kama Malecela na wengineo ndani ya CCM msaidieni maana anakokwenda ni kubaya
+1#14 mhogo mchungu 2011-01-10 11:26
kiukweli ccm na viongozi wake wanakera mno.Kwani hamna hata mtu wa kumuwajibisha huyo mama anayekosa adabu kiasi hicho.Ila kwa Makamba tumsamehe kwani ana matatizo mengi kwa wanaomfahamu vizuri watakubaliana na mimi sijui waliomchagua kwenye hiyo nafasi ya ukatibu mkuu walikua na malengo gani au walikosa mtu wa kumweka kwenye hiyo nafasi kwani naye ni kichefuchefu sana.kazi ipo.
+1#13 sig wa A town 2011-01-10 11:24
muwe na uelewa wanaccm kwamba pamoja na kuwa kazi kubwa ya viongozi wa dini ni kulisha watu chakula cha kiroho pia ni misingi ya kila dini kusimamia suala la aman ndio mana hua tunaimba amani kila kukicha.asa suala la maaskofu walikua sahihi kabisa kwa maana wasinge weza kufumbia macho suala la uvunjifu wa aman unaosababishwa na [NENO BAYA] wachache wenye uroho wa madaraka.nini itakua faida ya dini kama sio kuleta amani?na amani inaletwaje?ni kwakutofumbia macho mabaya yote yatokeayo chini ya jua. tafakari
0#12 Grace Andrew 2011-01-10 11:20
Nguvu na sauti ya umma isipo kadiriwa na wazee wa Taifa, Tuta kumbwa na Tsunami ya mabadilko kuwanzia Kalamu hadi sheria mkononi . kwa sbb Wana siasa wamefilisika ki Akili. Hiyo issue ni ndogo ukilinganisha na kwengine mambo ya ukabila na ubaguzi KM.IVORYCOAST, SOMALIA, IRAQI na hata hapo jirani.
#11 mwita mwita 2011-01-10 11:07

Tags:

0 comments

Post a Comment