Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameonya kwamba Sudan Kusini haitokuwa tulivu ikiamua kupiga kura ya kujitenga na kaskazini katika kura za maoni.
Aliiambia televisheni ya al-Jazeera kuwa kusini haina uwezo wa kuunda taifa thabit au kuwahudumia wananchi wake.
Mwandishi wa BBC James Copnall mjini Khartoum alisema kauli hiyo itawakera sana waliokuwa waasi wa SPLM ambao wamekuwa wakiiongoza kusini tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika mwaka 2005.
Mikutano ya mwisho imekuwa ikifanyika upande wa kusini kabla ya kura kuanza siku ya Jumapili.
Waandishi wanatarajia kura ya “ndio” kwa kishindo, itakayosababisha kuzaliwa kwa nchi nyingine duniani.
Kura hii ya maoni ni sehemu ya makubaliano ya mwaka 2005 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo miwili baina ya kaskazini na kusini.
0 comments