Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Arusha: Makamba amruka Chitanda sakata la Maaskofu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
CHAMA cha Mapinduzi kimemshukia katibu wake wa Mkoa wa Arusha Mary Chatanda kwa kauli yake iliyotafsiriwa juzi na Kada wa chama hicho John Malecela kuwa ni utovu wa nidhamu kwa maaskodu.

Mwishoni wa juma lililopita, katibu huyo aliwataka maaskofu mkoani humo kutoingilia masuala ya siasa vinginevyo wavue majoho na kujiingiza kwenye siasa.

Chatanda ambaye  ndiye chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa  mkoani humo  hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa.

"Tunawaheshimu sana viongozi wa dini, ila wanapoingilia masuala ya siasa ni bora wavue majoho tukutane viwanja vya siasa kama alivyofanya mwenzao Dk Slaa," alisema Chatanda.  Jana Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alisema kuwa kauli hiyo ni ya Chatanda mwenyewe na sio msimamo wa CCM.

"Unajua kijana alichoongea Chatanda  sio msimamo wa chama. Chama kina taratibu zake kabla ya kutoa tamko," alisema Makamba na kutaja Kamati kuu kuwa ndio yenye mamlaka ya kujadili jambo na kutolea tamko.

Aliongeza kuwa kila chama kina taratibu zake katika utoaji wa maamuzi kwa upande wa  CCM nayo ina taratibu zake ambazo zinatakiwa kufuatwa ikiwa ni pamoja na kukaa kikao cha kamati kuu ili kutoa kauli moja ikiwa kumetokea jambo fulani la kujadiliwa. 

Kauli hiyo ya Makamba aliitoa akiwa anajibu kauli ya Waziri Mkuu mstaafu , John Malecela ambaye alidai Chama Cha Mapinduzi kiwaombe radhi maaskofu baada ya kuwataka  wavue majoho na kuingia kwenye siasa.  Malecela alisema kuwa huo ni utovu wa nidhami uliofanywa na chama hicho hivyo kinachotakiwa ni kuomba radhi maaskofu hao.  Malecela ambaye pia ni kada wa CCM ,wakati anaitoa kauli yake hiyo alionekana kukasirishwa na hatua ya chama hicho kwa viongozi hao wa dini.

Januari 7 mwaka huu, maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha, walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba "hawatampa ushirikiano".  Walitoa tamko hilo wakati wakilaani hatua ya polisi mkoani Arusha kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

Akisoma tamko la umoja wa viongozi wa dini ya Kikristo mkoani Arusha, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu alisema Jeshi la Polisi ndilo lilikuwa chanzo cha vurugu hizo.  "Sisi kama viongozi wa dini hatuwezi kushirikiana na mtu ambaye hakushinda kihalali, kuna mtu alipiga kura si diwani wa Arusha, Chadema hawakushirikishwa na pia taratibu na kanuni za uchaguzi huo zilikiukwa," alisema askofu huyo.    


Sent from my iPhone
Tags:

0 comments

Post a Comment