Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mzozo mpya wa kidiplomasia waibuka kati ya Marekani na Venezuela

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Mzozo mpya wa kidiplomasia kati ya Marekani na Venezuela umezuka baada ya Marekani kufutilia mbali visa ya balozi mpya wa Venezuela  Bernardo Alvarez. Hii ni baada ya Venezuela kukataa uamuzi wa Marekani kumteua Larry Palmer kuwa balozi wake mpya Venezuela. Wakati baraza la Seneti la Marekani, lilipokuwa likisikiliza maelezo ya Palmer kabla kumuidhinisha rasmi, balozi huyo mteule aliilaumu serikali ya rais Hugo Chavez wa Venezuela kwa kuhifadhi waasi wa upinzani kutoka Colombia. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kufutwa kwa visa ya Alvarez ni kulipiza hatua ya Venezuela kumkataa Palmer.
Tags:

0 comments

Post a Comment