Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Baada ya watu 6 wa Familia moja ya Kigogo TLP Kuteketea, Mrema aja juu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Na Joseph Ngilisho, Moshi 
Kufuatia watu wasiojulikana kuchoma moto nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Andrew Anselim Lekule (50) na kusababisha vifo vya watu wawili , Catherine Lekule (45) na mwanaye Flora Lekule (6),  jeshi la polisi limewatia mbaroni watu sita.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ngh’oboko aliliambia gazeti hili kuwa, kufuatia tukio hilo lililotokea Desemba 13, mwaka huu, linawashikilia watu sita akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyala kabla ya kuvuliwa madaraka, Augustine Fabian Kessy .

Aliwataja wengine kuwa  ni Augustine Mrema (42), Philipo Aloyce (24), Severine Abrose (45), Cosmas Augustine (40) na Augustine Shayo (24) wote wakiwa ni wakazi wa vijiji mbalimbali katika Jimbo la Vunjo.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti ambaye amenusurika kifo alisema  kuwa, amepoteza mkewe na mwanaye ambao waliungua vibaya kiasi cha kutotambulika  baada ya juhudi za kujiokoa kushindikana.

Lekule alisema kuwa, tukio hilo limemuacha katika mazingira magumu kutokana na mali pamoja na pesa kuteketea.

Akisimulia mkasa mzima Lekule alisema; “Kabla ya tukio hilo, nilisikia kishindo kikubwa nje, ilikuwa  saa 4 usiku baada ya kutoka kwenye ulinzi wa sungusungu, wakati najiandaa kufungua mlango nikasikia sauti nje ikiniambia ‘toka uone’.
“Wakati bado najishauri cha kufanya, ghafla nilisikia sauti kubwa ya mlipuko ikiambatana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka juu ya paa la nyumba yangu.

“Nilifanya jitihada za kujiokoa mimi na mwanangu mmoja lakini moto huo ulichukua uhai wa mke wangu na mwanangu mmoja, niliumia sana.

“Baadaye, jitihada za kuwasiliana na polisi zilifanyika na hata walipofika walikuta moto huo umeshateketeza kila kitu, ndipo walipoingia ndani na kukuta miili ya marehemu hao ikiwa imeungua vibaya.”

Akiongea na Uwazi nyumbani kwake kijijini hapo, Mbunge wa Vunjo Mhe. Augustine Mrema (pichani) alisema kuwa, tukio hilo limetokana na njama zilizofanywa na kundi la watu wahalifu sugu.

“Hili tukio limenisikitisha sana na najua waliofanya hivyo ni wahalifu sugu ambao mimi na bwana Lekule tumeamua kuwashughulika lakini hatutakata tamaa, tumeapa kufa nao,” alisema Mrema.
Tags:

0 comments

Post a Comment