Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wabunge wamkalia kooni Chenge. Wamwagia Sifa Kemkem SITTA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter WABUNGE wateule wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wamemkalia kooni Mwanasheria Mkuu wa zamani Serikali anayewania kuteuliwa kugombea uspika wa Bunge kupitia CCM, Andrew Chenge kwa kumshambulia Samuel Sitta akisema kuwa uongozi wake ulijenga makundi ndani ya Bunge na hakuwa upande wa serikali.
Mbunge mteule wa Mbozi Mashariki(CCM), Godfrey Zambi alisema Bunge la Tisa lililomaliza muda wake lilikuwa na changamoto kubwa katika kukuza demokrasia bungeni iliyowafanya Watanzania walipende, hivyo spika anayehitajika ni yule atakayeendeleza uhuru huo wa kutoa hoja bila upendeleo.

“Spika na naibu wake waliliendesha Bunge kwa viwango kweli kweli, hivyo watakaofaa kuchukua nafasi hizo lazima wawe na sifa za aina hiyo ili kuiimarisha serikali ya CCM katika kipindi hiki cha miaka mitano,” alisema Zambi.

Dk Festus Limbu ambaye ni mbunge mteule wa Magu CCM, alisema kuwa Spika anayehitajika ni yule atakayeweza kusimamia mihimuli mitatu ya serikali na ambaye hatayumbishwa na chama tawala wala upinzani.

“Kutokana na ujio wa vijana wengi na upinzani mkubwa ni wazi kuwa ni changamoto kwa serikali ya CCM, hivyo Spika anayetakiwa ni yule atakayeweza kukubaliana na hali hiyo na kutoegemea upande wowote,” alisema Dk Limbu.

Naye mbunge mteule wa Kahama (CCM), James Lembeli aliungana na waliomtangulia akisema sifa za spika ziwefanane na za uongozi uliopita.

Lembeli alisema hata wakisema kuwa kuna mwingine lakini, kazi aliyoifanya Sitta imeonekana na kwamba hata mambo ya mtandao yanayozungumzwa hakuna.

“Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,” alisema Lembeli.

Naye mbunge mteule wa Longido CCM, Lekule Laizer alisema Spika anayehitajika awe ni mwenye uweza kusimamia ukweli na maslahi ya nchi bila kupendelea kikundi au chama chochote .

“Tunataka spika anayeweza kusimamia maslahi ya taifa bila kuwa na vikundi na kupendelea upande mmoja,” alisema.

Mbunge mteule wa Ngorongoro Saningo Telele ( CCM) hakutofautiana na Laizer kwa kueleza kuwa spika anayehitajika ni yule atakayesimamia kwa dhati muhimili wa Bunge na maslahi ya Watanzania kwa ujumla.

Mbunge mteule wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF) alisema kuwa tangu Bunge lianza baada ya uhuru kumekuwa na maspika wengi, lakini sifa kama za Spika Sitta ndizo zinazohitajika.

“Sitta ndiye mwenye sifa za Spika hakuna mwingine na ana viwango, ni mtu mkakamavu na nasisisitiza sifa za Sitta ndizo za spika anayeweza kuhimili pande zote ndani ya Bunge,” alisema.

Paul Lwanji mbunge mteule wa Manyoni Magharibi CCM, alisema anahitajika Spika mwenye kasi na viwango. Hata hivyo alisema kitendo cha wengi kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili kwania nafasi hiyo ni haki yao ya kidemokrasia.

Mbunge mteule wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) alisema CCM inajua sifa za Spika anayehitajika na wananchi hivyo wajiulize nani anafaa kusimamia mhimili huo dola kwa umakini.

“Kila mmoja ameomba kuwania nafasdi hiyo hilo ni suala la demokrasia, lakini hatuwezi kuwa na spika ambaye hafai kabisa na sifa zake ni mbaya, hivyo kosa lisifanyike kwani linaweza likaleta matatizo makubwa,” alisema Shibuda.

Dk Athuman Mfutakamba mbunge mteule wa Igalula CCM, alisema kuwa anahitajika Spika atakayesimamia taratubu na shughuli zote za bunge viziri kwa busara na hekima.
Tags:

0 comments

Post a Comment