You Are Here: Home - - Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Polisi nchini inashirikiana na Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ili kubaini wahusika wa mtandao wa gazeti tando la zeutamu. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Msemaji wa Polisi, Juma Said Ally, alisema Polisi inashirikiana na Interpol ili kubaini wamiliki wa mtandao huo.
Alisema wanaamini wahusika wapo ndani na nje ya nchi na hivyo wameamua kushirikiana nao ili kuwakamata na sasa wanaendelea na uchunguzi. “Tunashirikiana na Interpol ili kuwakamata wahusika wanaodhalilisha viongozi na watu mbalimbali na tunaamini wahusika hawa wapo ndani na nje ya nchi, hivyo tunaendelea na uchunguzi,” alisema.
Hatua hiyo ya Polisi kusaka wahusika wa mtandao huo inakuja baada ya wananchi kukerwa na udhalilishaji unaofanywa na wahusika hao kupitia mtandao huo. Siku za karibuni mtandao huo umekuwa ukitumia nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari kudhalilisha viongozi, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya jamii na uandishi wa habari.
BONY HII NEWS MBONA ISHAKUA KIPORO KILICHOPOA, SI ALISHAKAMATWA? AU KUNA WENGINE WANAO TAFUTWA?