Katika majumuisho yake, mwanansheria wa Ghailan, Peter Quijano,amesema waendesha mashtaka wa Marekani walikuwa hawana udhibitisho kuwa mtanzania huyo alifahamu kwamba alikuwa akisaidia kupanga njama za mashambulio hayo yaliyosababisha vifo vya watu 224.
Naye mwendesha mashtaka wa serikali, Michael Farbiarz ,alisema kuwa Ghailan mwenye umri wa miaka 36 ni mwongo na kwamba alikuwa mwanachama wa mtandao wa Al-Qaida aliyekuwa akilipwa na kuhusika na mashambulio hayo.
Ghailan alikamatwa nchini Pakistana mwaka 2004, na kupelekwa katika jela ya siri ya shirika la ujajusi la Marekani CIA kabla ya kuhamishiwa katika jela la Guantanamo Bay.

0 comments