IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Ni kituko na aibu tupu kwa mastaa wawili waliokuwa wapenzi wa kufa na kuzikana, muigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na mwanamuziki Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ ambao wamefikia uamuzi wa kuachana kwa kashfa na kutoleana maneno ‘mbofu mbofu’ hadharani, Ijumaa linakupa kitu kamili.
Katika makabrasha ya Ijumaa, kuna data zisizohitaji chanzo kwani ‘sosi’ ni wahusika wenyewe ambao wamekuwa wakifanyiwa mahojiano na gazeti hili kwa nyakati tofauti huku Jini Kabula akiwa kinara wa maelezo akidai kumtapika Mr Nice na kuanika uchafu wake.
Kwa mujibu wa Jini Kabula, haoni umuhimu wa kuendelea kuwa na Mr Nice kimapenzi kwa sababu suala hilo analichukulia kama gunia la misumari alilojitwisha kichwani huku akiwa na upara.
Jini Kabula, bila koma, nukta wala simile, alikuwa na haya ya kusema: “Nashangaa watu wanaosema namuonea wivu Mr Nice kwa sababu nimeachana naye hivyo anapokuwa na mwanamke mwingine roho inaniuma, siyo kweli kwani mimi ndiye niliyemrudisha Nice kwenye chati, alikuwa ametoweka katika anga ya muziki, alipoanza kuwa na mimi kimapenzi, ndipo akasikika na kuanzisha Bendi ya Bush.
“Nice (Mr) alipoanza kuwika tu, ndipo akawa kinara wa kubadilisha mashori kila kukicha na mimi kuambulia kipigo cha kufa mtu.
“Ijulikane kuwa nimeanza mapenzi na Nice akiwa na suruali na shati moja tu, kula kwenyewe ilikuwa tabu, nilitumia kipato cha kazi zangu za usanii ‘kumfufua’, mbaya zaidi, mwenzangu alipokuwa akipata pesa alikimbilia kwa wanawake tena wengine ni rafiki zangu kabisa.
“Nimeamua kumtapika Mr Nice liwalo na liwe, mwanaume gani kashindwa hata kunitimizia mambo kadhaa kwa kipindi chote nilichoishi naye.
“Niligombana kila kukicha na wanawake wenzangu, kuna mwanamke mmoja aitwaye Lulu ambaye tuligombana sana. Baadaye niligundua kuwa Lulu hakuwa na kosa, nilimtafuta tukakaa chini na kukubaliana kuwa Nice anatuchanganya akili, tukaamua tuelewane kwani sisi wote ni wanawake.
“Tukio bichi ni la mwanamke mwingine wa Mr Nice anayeishi naye Tandale Kwamtogole, Dar, anaitwa Najma na amekuwa akinitumia vitisho mimi na Lulu hivyo tumeamua kumripoti polisi na kesi inakwenda mahakamani ili kieleweke,” alimalizia Jini Kabula huku akiwa na jazba.
Baada ya kumsikia Jini Kabula, Ijumaa lilimwendea hewani Mr Nice ambaye yuko jijini Mwanza kikazi ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Sitaki kuzungumza chochote, ieleweke kuwa Kabula na wenzake wote wamepinda. Watajijua wenyewe mimi sihusiki.”
Akiongea juu ya ishu hiyo katika kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kunako Radio Times ya Dar, Jini Kabula alimshangaa Mr Nice kwenda kuishi Tandale, jambo lililosababisha wakazi wa eneo hilo kukasirika na kuahidi kumsaka kila sehemu kwa kuwakashfu.
You Are Here: Home - - Scandal ya Mr. Nice na Mademu zake
0 comments