Uingereza na Ujerumani zaunga mkono mazungumzo ya amani
London:
Uingereza na Ujerumani zimeyaunga mkono mazungumzo ya amani ya ana kwa ana kati ya Israel na Palestina, yalioanza leo mjini Washington, na kuonya kwamba kushindwa kutakuwa na athari kubwa. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague na mwenzake wa Ujerumani Guido Westerwelle, wamezitaka pande hizo mbili zijitolee na kuonyesha nia ya kuleta mafanikio, na kuongeza kuwa Umoja wa Ulaya uko nyuma yao.Waziri Westerwelle ameyaita mazungumzo hayo kuwa ni nafasi ya moja kwa moja ya kuleta mafanikio," lakini akaonya kwamba wafuasi wa siasa kali katika Mashariki ya kati watajaribu kuhujumu maendeleo yake.
Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ambayo yameanza mjini Washington ni ya kwanza baada ya miezi 20.
0 comments