Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Uganda yasisitiza EAC ya sasa ni imara

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter NAIBU Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eac) wa Uganda, Eriya Kategaya amesema nchi tano zinazounda jumuiya hiyo zimeweka msingi imara kuhakikisha kwamba haivunjiki tena.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Masuala ya Umma ya Eac, jana ilimnukuu Kategaya akifafanua kwamba miaka 10 baada ya mkataba ulioanzisha upya jumuiya hiyo kutiwa saini, Eac imenufaika sana katika kuimarisha kuaminiana na nia njema miongoni mwa wanachama wake.

Jumuia ya awali ilikufa mwaka 1977 ikiwa ni miaka 10 tu baada ya kuanzishwa kwake kutokana na pamoja na mambo mngine tofauati za kisiasa, kichumi na kiitikadi miongoni mwa wanachama wa wakati ule ambao ni Kenya, Uganda na Tanzania. Jumuiya ya sasa imepata wanachama wengine wawili ikiwa ni pamoja na Rwanda na Burundi.

‘’Kwa mfano Jumuiya ya sasa ina mizizi yake kutoka kwa jamii na ina msukumo wa soko huria; mamlaka yamekasimiwa kutoka kwa wakuu wa nchi kwenda kwa mawaziri, jumuiya za kiraia, serikali za mitaa na sekta binafsi,’’ alisema.

Kategaya alikuwa anafungua rasmi warsha ya kuhamasisha wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wasio wanataaluma katika Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala, Uganda mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Jumuiya hiyo kuelimisha umma juu ya shughuli zake katika kanda nzima.

Wajumbe wapatao 100 waliohudhuria warsha hiyo ikiwa ni pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo wa Kwanza wa Chuo hicho, Profesa Lilian Tibatemwa-Ekirikubinza walielezwa kwamba kutokana na ushirikiano huo, ukusanyaji mapato nchini Uganda umepanda kutoka dola 300 milioni za Marekani mwaka 2005 ilipofufuliwa Jumuiya hiyo hadi kufikia dola 650 milioni kwa mwaka ilipofika mwaka 2008/9.

Katika warsha hiyo pia Naibu Katibu Mkuu wa Eac anayeshughulikia shirikisho la Kisiasa, Beatrice Kiraso alisisitiza kwamba ushirikiano wa kikanda ni muhimu na siyo jambo la hiari akitoa mfano wa mwenendo wa dunia hivi sasa ambao unazitaka nchi ziimarishe ushirikiano miongoni mwao zikiwemo nchi zenye nguvu zaidi duniani kuliko za Eac.
Tags:

0 comments

Post a Comment