Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Zimbabwe yaunga mkono nyuklia za Iran

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameunga mkono 'kusudio halali' la Iran kutengeneza nishati ya nyuklia.
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad anamalizia na ziara yake nchini Zimbabwe. Rais huyo baadaye ataelekea Uganda.

Kiongozi huyo wa Zimbabwe amesema nchi yake pamoja na Iran 'zimekashifiwa na kuadhibiwa visivyo halali na nchi za Magharibi'.

Iran inakabiliwa na vikwazo vya kibiashara na kidiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa, ingawa nchi hiyo imesisitiza kuwa miradi yake ya nyuklia sio ya kutengeneza silaha.

Bw Ahmadinejad anatazamiwa kufungua maonesho ya biashara mjini Bulawayo.

Hata hivyo chama cha waziri mkuu Morgan Tsvangirai,MDC, kimelaani ziara hiyo, na hakikutuma mwakilishi yeyote kwenda kumpokea rais wa Iran alipowasili.

Chama hicho kimesema kumualika rais huyo kufungua maonesho ya biashara, ni sawa na 'kualika mbu kutibu malaria'
Tags:

0 comments

Post a Comment